top of page

Tunza usichana wako, utimize ndoto yako

Updated: Apr 17

Msichana hapana yako leo ndiyo usalama wa maisha yako ya sasa na yajayo


Na Mwinjilist Elisa Kaimukilwa


Msichana ni miongoni mwa watu ambao wako kwenye hatari ya kuharibiwa ndoto za maisha yake kama hatojitambua.

 

Kutokujitambua kwa msichana kumekuwa kukichangiwa na sababu mbalimbali ikiwemo kubarehe, hiki ni kipindi kibaya sana kwa msichana kwa sababu hujiona tayari ni mtu mzima mwenye kuweza kufanya kila kitu bila kuhitaji msaada wa mtu yeyote.

 

Mfano; kipindi hiki huwa na majibu yasiyo rafiki, ubadilisha hata tembea, uanza kujijali sana hasa kwa kujiremba kama kusuka, kupaka rangi, manukato, usafi uliopitiliza na hupenda kujifunza mapishi ya vitu mbalimbali.

 

Kudekezwa pasipo yeye kujua maisha yanayofuata yanamuhusu yeye tu bila mtu mwingine, hapa unakuta mzazi anashindwa kumpitisha kwenye misingi bora ya maisha yajayo.

 

Kutokana na mabadiliko anayokuwa nayo ujikuta akifuatiliwa na vijana wa kiume na hata wanaume  watu wazima kwa lengo la kuwa naye kwenye mahusiano na nia yao ikiwa sio njema ikiwemo kuharibu ndoto za maisha ya wasichana hao, uwadanganya kwa kuwapa vitu vidogo vidogo kama pesa, nguo pia kuwadanganya na maneno mazuri.

 

Utasikia wakisema “wewe mzuri kama malaika” wakijua kabisa kuwa atashawishika, msichana anaposikia maneno hayo yanamvuruga akili na mfumo wote wa akili.

 

Na wengine uenda mbali zaidi na kusema “nitakuoa ila nataka umalize shule kwanza” yaani kusikia hivyo anaona mwanaume huyo ni mzuri na ana malengo naye, kumbe hayoyote ni chambo katika ndoano  pia vizawadi vizuri vya aina mbalimbali na  vingine vya gharama kubwa upewa. 

 

Kwa ulaghai huo kama msichana atakuwa hajajitambua na kujua yuko katika hali na mazingira gani ni rahisi kunaswa na chambo na ukawa mwanzo wa kupoteza ndoto zake.

 

Msomaji bila shaka unaweza kuwa shahidi wa jambo hili, wapo waliopelekwa shule lakini wakajiingiza kwenye makundi mabaya na kuharibu ramani ya maisha yao na sasa wanajuta kukosa elimu wakitamani kama wangepata fursa nyingine ya kurejea shule lakini wakuwasomesha hawapo tena.

 

Msichana, ngoja nikwambie na nikukuonyeshe ulivyo wathani, HAPANA yako ndiyo usalama wa maisha yako ya sasa na yajayo kwa sababu ukiwa na msimamo wa HAPANA unakujengea kuogopwa, kukubaliwa, kuheshimiwa, kuthaminiwa kwa maana watasema "yule msichana uwa anamsimamo kweli kweli".

 

Msichana baada ya kukataa, kwa kumshusha thamani utamsikia mwanaume akiongea maneno ya kejeli kwa kusema, “anamsimamo lakini si mzuri, hajasoma sijui ataolewa na nani kama hataki kuongea na sisi”, maneno haya yanaweza kukufanya kwa mpweke na kumbe ni mbinu za kunasa ili kuharibu ndoto zake.

 

Kijana au mwanaume yuleyule alivyo wa ajabu akikuhitaji kimahusiano ukakubali, utasikia mguno(mmmh) “huyu ni ovyo kabisa, yaani nimemwambia tu sijakamilisha neno akawa tayari amekubali,  hamna kitu kabisa!”, Jiulize swali la msingi amesema anataka kukuoa, kwanini anataka tendo la ndoa kabla ya kufunga ndoa? Kwani ni chakula kusema anaonja chumvi au chai anaonja sukari?

 

Usimuone kila kijana aliyembele yako kuwa ni mzuri kwako, nataka nikwambie kuwa kila jambo lina wakati wake, hakuna hatua ambayo utairuka, hatua zote utazifikia jilinganishe na mtoto mdogo aliye zaliwa hawezi kutembea kwa muda huo huo lazima kuna hatua anazozipitia, atafundishwa kukaa hata kwa kuwekewa nguo kwenye beseni, atatambaa, atashikwa mkono ili etembee, atakimbia, na kwa mantiki ya kawaida ni ngumu kujifunza kukaa na wakati huo akakimbia.

 

Hivyo kijana huyu kuondoka usoni mwako hata kama ana maneno mazuri sana sio kwamba maisha yako yameishia hapo, laasha maisha yako yapo kwa kulindwa na wewe, usitumie kigezo cha kufikisha miaka 18 kuharibu maisha yako.

 

Jua kwamba akikupa mimba, anayebaki kutaabika ni wewe mwenyewe, kijana au mwanaume anabaki salama katika jamii bila changamoto yeyote lakini kwako inabaki kuwa fedheha na kupoteza dira ya maisha yako.

 

Na pengine ukihitaji msaada wake baada ya kupata mimba, anakunyima ushirikiano na ukijaribu kumtafuta hata kwa kumpigia simu anaweza asipokee au na hata akipokea ukamwambia kuhusu mimba utasikia akisema “weeee koma kabisa mimba yangu!!!, nitolee kabisa, kama ulijichanganya shauri yako”, namajuto uanzia hapo ukianza kumkumbuka maneno mazuri aliyokuwa akikwambia na ahadi zake za uongo alizokuwa akikupatia kabla ya kupata mimba

 

Hapa ni lazima ukumbuke jinsi wazazi, walezi au waalimu wako walivyokuwa wakikwambia na kukukanya japo haiwezi kukusaidia tena maana yamepita, maana ulivyoyaona.

 

Ebu angalia kijana huyu amekuja njia ya nitakuoa umekubali, mwingine amekuja hivyo umekubali kadhali na mwingine, jiulize kwa hali ya kawaida unaweza kuolewa na watu watatu kweli kwa kipindi kimoja, tafadhali tunza usichana wako maana niwa thamani sana si kwamba kijana anakuharibia ndoto zako tu pia unaweza kuwa maradhi kama magonjwa ambukizi kama HIV, nahuenda yakakuachia madhara yakudumu.

 

Kumbuka ili uwe salama epuka mambo haya, kujirahisha kwa kila mtuanayepita mbele yako, tamaa ya mambo makubwa, kusikiliza kila maneno unayoambiwa pasipo kujiridhisha, kugeuka nyuma ovyo kwa sababu ya miruzi inayopigwa.

 

Pia maneno ya kukatisha tamaa kama wanawake ni wengi kuliko wanaume, kuufanya mwili wako kuwa kitega uchumi, elimu yako ya juu kukuponza kuona huwezi kufanya kazi ndogondogo kama kuuza karanga, dagaa kisa umemaliza kidato cha sita au chuo.

 

Jua anayekutamani, kukuhitaji na kujifanya rafiki yako leo ndiye adui yako wa kesho baada ya kuwa umeshapata matatizo, unavyo angaika kupata 100 katika mitihani basi angaikia maisha yako mpaka kutimiza ndoto zako; Ukweli ni kwamba vijana hawawapendi bali wanawatamanikuwa nao kwa muda tu, asilimia kubwa ni waongo.

 

 

Kijijini kwetu msichana alikuwa na urafiki wa kimapenzi na kijana, juma pili moja wakatembea, jua likazama na usiku ukaingia msichana akaogopa kwenda kwao akamwambia kijana kwamba muda huu siwezi kwenda nyumbani lazima inipeleke kwenu yaani mimi leo nimeolewa, kijana akajifikiria kama dakika 2 akamwambia sawa twende.

Walipo karibia nyumbani kwao kijana, akamwambia msichana waingie kichakani wafanye tendo la ndoa baadae waende, msichana kwakuwa ameshajiaminisha akakubali, baada ya kumaliza wakaenda na walipoingia ndani kijana akaingilia mlango wa mbele na kutokea mlango wa nyuma na kukimbia.

 

Siku ikapita pasipo kijana kuonekana, wazazi wake wakamwambia msichana kuwa aende kwao kwani aliyemleta haonekani, basi msichana ikabidi aondoke, Tujiulize kwa nini wawili hao waliamua kupita kichakani? Kwani walichoenda kufanya kichakani si ni kile ambacho wangefanya nyumbani? Uharaka ulikuwa wa nini?

 

Ona sasa, msichana ameishajidharirisha na ndoa haipo tena, na kibaya zaidi hata aliporejea nyumbani binti huyo akafukuzwa, doto zake zimeharibika na wengine wanakuhesabu kuwa uliolewa siku moja na ukaachika siku hiyo hiyo na hayo ni majonzi ya tamaa ya mwili.

Ewe msichana haya unapaswa kuyafanya si kwa kuwahurumia wazazi jiurumie wewe na maisha yako ya baadae linda moyo wako kuliko yote uyalindayo.

 

Tambua kuwa usichana wako ni lulu ya thamani sana kama ambavyo utaki kitu chochote kikuingilie kwenye jicho lako basi usiruhusu mtu yeyote aingilie maisha yako na kukuharibia ndoto yako.

 

Hata kama hutambui wewe ni taifa tegemewa leo mpaka kesho watakutisha, watakukejeli na kukudharau watakusema vibaya, vyovyote vile kuwa makini sana na maisha yako maana ndiyo ufunguo maisha yako ya kesho jua baada ya kuanguka walewale watakucheka huruma yao ya kejeli haitainua maisha yako bali itakuwa ni AIBU itakayokufanya ukose kujiamini, kumbuka aliyekuumba anakuwazia mema daima.

 

Jipange dhidi ya maisha yako ya mbele nahusitoke kwa wazazi wako kwa sababu wanakuulizia juu ya maisha yako ukafikiria ni bugudha mfanoukiulizwa juu ya kwanini umechelewa kuja nyumbani?, Umeacha nani apike? Na au ukaulizwa juu ya hao niakina nani wanaokusahaurisha majukumu yako?

 

Unatakiwa kutambua kuwa wazazi au walezi hawakuulizi kwa nia mbaya ni katika kukujenge msingi mzuri wa maisha yako ya baadaye.

 

Pia husifikirie kuwa, kwa kuwa umepata wa kukulipia kodi anakupenda la hasha naye kuna namna anavyotaka kuchezea maisha yako, hakikisha kuwa unapo taka kutoka kwenda kujitegemea una hakika ya kula na kunywa na kuyaweka maisha yako kuwa salama angalau 90%, ukiwa tegemezi kwa mtu ambaye hana huruma na wewe utapoteza maisha yako na thamani ya usichana wako itaaribiwa na kuharibika.

 

Comments


bottom of page