top of page
word-team-scrabble-letters-black-backdrop.jpg

MONTESSORI TANZANIA - Montessori For All

Elimu ya Montessori inazingatia kuwa kila kitu kinachokuzunguka ni elimu

Gazeti la MONTESSORI TANZANIA ni mpango endelevu wa kukusanya, kutumia, kuhamasisha na kupasha habari chanya hususani juu ya malezi, elimu na makuzi na kuangazia ukuaji wa matumizi ya lugha rafiki, mbinu shirikishi na elimu kwa vitendo katika kubaini, kulea, kuibua fikra tunduizi na kukuza vipaji chanya na kujenga matendo ya kiutu na kiuzalendo kupitia hatua zote za makuzi ya mwanadamu na kuangazia changamoto zinazoweza kupelekea kutofikia malengo  katika kulea, kujitegemea, hali ya ujifunzaji na ufundishaji na kuyatafutia ufumbuzi kwa wakati ili ifikapo mwaka 2035 taifa liwe na watanzania wengi wanaotambua umuhimu wa matumizi ya lugha rafiki, zana wezeshi na mbinu shirikishi katika mawasiliano, ujifunzaji na ufundishaji.
 
Gazeti pia litawasaidia wadau kupata taarifa zinazowawezesha kuwa na utashi na kushiriki moja kwa moja katika kuboresha miundombinu ya elimu na malezi bora.

Pamoja na wingi wa taarifa zinazopatikana kwa kuwezeshwa na vyombo mbalimbali ya habari hapa nchini, Jamii ya kitanzania imekuwa ikipata changamoto ya upatikanaji wa chombo cha taarifa chenye habari endelevu za Elimu na Malezi za moja kwa moja zinazohusiana na utatuzi wa changamoto zinazojitokeza katika jamii zetu za mmomonyoko wa maadili, namna bora ya kulea, namna sahihi ya kushauri vijana, fikra tunduizi na chanya,ukuzaji wa stadi za KKK na ukuzaji vipaji, ili kuendeleza na kudumisha misingi ya utamaduni wa Kitanzania na kuenzi uzalendo, na namna bora na sahihi ya  utangamana na nchi za kikanda na mataifa mengine kwa kuzingatia maadili ya kitanzania.

Timu Yetu

madame_edited.jpg

Jacqueline Mwombeki

CEO Mkurugenzi Mtendaji wa Montessori Tanzania

Huyu ndiye mkurugenzi mtendaji wa gazeti la Montessori Tanzania. Ndoto yake ni kuona wazazi, walezi na walimu, wanatumia mbinu na falsafa za Dr. Maria Montessori kama mbadala katika kuboresha ujifunzaji na ufundishaji mashuleni na kwa kuwalea watoto katika misingi ipasayo kabla hata ya kuanza kuwarekebisha kimienendo na kitabia. Hapa mzazi atabaini mbinu na namna ya kumwezesha mtoto kukua kiukamilifu kumtoa kwenye hali tegemezi na kutojiamini ambavyo pengine mazingira yanakuwa tayari yamemjengea, na kumrudisha kwenye uasili wake ambao ni kujitegemea kifikra, kimawazo, kimatendo na uthabiti katika kufanya maamuzi. Gazeti hili limeanzishwa kutoa mchango katika ukuzaji na uenezaji wa falsafa za Dr. Maria Montessori kwa kuwawezesha walimu wa kimontessori walio tayari kufundisha kwa mfumo huo ambao Jacqueline anasema ameuhudumia mfumo wa Montessori takribani miaka 30 katika ufundishaji watoto na watu wazima mkoani Kagera kwa ufanisi mkubwa sana na kubaini kuwa hapajawahi kuwepo mfumo mzuri zaidi, rafiki na shirikishi kwa watoto katika kuwapatia elimu mashuleni kama ilivyo kwa Montessori. “Tunatambua kuwa kizazi cha karne ya 21 ni kizazi cha mwendo kasi kwa maana ya ukuaji wa teknolojia ambapo unakuta wazazi hawana muda mwingi wa kukaa karibu na watoto wao kulingana na shughuli mbalimbali za kiuchuminaza kijamii ili hali mtoto akiwa analelewa na watu wengine wasio ujua uchungu wa mtoto huyo.” Jacqueline anaamini kuwa kupitia makala za “Elimu na Malezi,” kila msomaji ataondokana cha kwake kwa upande wa makuzi, mbinu na falsafa, kadhalika elimu zitakazokuwa zinatolewa na waandishi mbalimbali wa gazeti hili pamoja na kupata burudani. Jacqueline anasema; anayo matarajio kuwa kupitia mkakati huu mzuri unaotoa elimu kwa wote kwa lengo la kukomboa kizazi chetu, mabadiliko chanya yatakuwepo kwa kuanza na mtu mmoja mmoja.

FB_IMG_17158485422462402_edited.jpg

Arnold

KAILEMBO

Katibu Mtendaji

Natumikia gazeti la Montessori Tanzania kama Katibu mtendaji, Ni fahari yangu kuwa sehemu ya uzalishaji wa gazeti la Montessori Tanzania ambalo limejipambanua kwenye kuihudumia jamii katika nyanja mbalimbali kupitia habari makala zikilenga kuleta mabadiliko chanya katika Elimu, Malezi na Makuzi. Tunavyo vipengele mbalimbali vinavyomlenga kila mtu mtoto, kijana, mzazi na wazee, kupitia makala tunaelimisha, kukumbusha na kuonesha thamani ya mambo mbalimbali katika jamii, serikali na wadau. Ni imani yangu kupitia jukwaa hili utapata maarifa mapya, usahihi wa mambo pamoja na ukumbusho wa vitu muhimu kwako. Karibu uwe mmoja wa familia yetu kwa kujisajili sasa.

IMG_1974_edited.jpg

Steven G.

TOMAS

Msanifu wa gazeti

Mimi ni msanifu wa gazeti la Montessori Tanzania, kupitia kazi yangu kwa kushirikiana na timu nitahakikisha nazalisha kazi bora itakayomvutia na kumuhamasisha msomaji kuma mfuatiliaji wa makala zetu. Karibu uwe mmoja wa familia yetu kwa kujisajili sasa.

IMG_1978_edited.jpg

Ezra

MCHUNGUZI

Mlinzi

Mimi ni mlizi katika taasisi ya Montessori Tanzania, pamoja na kazi yangu ya ulinzi ni mfuatiliaji mzuri sana wa makala zinazotolewa ambazo kwa wingi zinatoa elimu ya kujithamini, kuthamini wengine na vitu katika jamii Karibu uwe mmoja wa familia yetu kwa kujisajili sasa.

IMG_9864_1x_2-2_edited.jpg

Kemilembe

NDYAMUKAMA

Mjumbe wa Bondi na Mshauri

Mimi kama familia ya Montessori Tanzania niwaalike vijana wa Tanzania, Afrika na Dunia kwa ujumla kuungana na Gazeti la Montessori Tanzania lililobeba maono makubwa na chanya yenye fursa katika kuelekea uchumi wa kijani. Gazeti hili linatuunganisha vijana kupitia makala zilizosheheni Elimu tofauti tofauti zitakazotuwezesha sisi kama vijana kutokomeza maadui watatu ambao ni Ujinga, Umasikini na Maradhi, Jambo litakalotufanya kufanikisha maono na malengo yetu kwa neema zake Mwenyezi Mungu, kwani tunapojielimisha kwa hiari kwa mambo mbalimbali, ni wazi kuwa tunakuza UWEZO WETU KIFIKRA NA KIMITAZAMO. Niliwahi kusoma kitabu cha nukuu za Kiswahili za Mwalimu JK Nyerere uk.152, aliwahi kusema kuwa moja ya ahadi ya Mwana TANU ni “Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu wote na kuitumia Elimu yangu kwa faida ya wote” mwisho wa kumnukuu. Hata hivyo sisi kama vijana tunao wajibu wa kujisomea vitabu na kurasa mbalimbali zenye maarifa chanya mtandaoni ambavyo vitatuondolea hali ya kuishi kwa mazoea na kuuishi uhalisia katika nyanja tofauti ikiwemo maadili, mila na desturi zetu. Hata kupitia Gazeti hili la Montessori Tanzania katika makala tunapata elimu na fursa zinazotuwezesha kujiamini na kujikwamua kimaisha. Karibu uungane nami KEMILEMBE J NDYAMKAMA na Gazeti la Montessori TANZANIA Gazeti hili linatuunganisha vijana kupitia makala zilizosheheni Elimu tofauti tofauti zitakazotuwezesha sisi kama vijana kutokomeza maadui watatu ambao ni Ujinga, Umasikini na Maradhi, Jambo litakalotufanya kufanikisha maono na malengo yetu kwa neema zake Mwenyezi Mungu, kwani tunapojielimisha kwa hiari kwa mambo mbalimbali, ni wazi kuwa tunakuza UWEZO WETU KIFIKRA NA KIMITAZAMO. Niliwahi kusoma kitabu cha nukuu za Kiswahili za Mwalimu JK Nyerere uk.152, aliwahi kusema kuwa moja ya ahadi ya Mwana TANU ni “Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu wote na kuitumia Elimu yangu kwa faida ya wote” mwisho wa kumnukuu. Hata hivyo sisi kama vijana tunao wajibu wa kujisomea vitabu na kurasa mbalimbali zenye maarifa chanya mtandaoni ambavyo vitatuondolea hali ya kutokuishi kwa mazoea na kuuishi uhalisia katika nyanja tofauti ikiwemo maadili, mila na desturi za kitanzania na za kiafrika. Hata kupitia Gazeti hili la Montessori Tanzania katika makala tunapata elimu na fursa zinatuwezesha kujiamini na kujikwamua kimaisha. Karibu uungane nami KEMILEMBE J NDYAMKAMA na Gazeti la Montessori TANZANIA

IMG-20240815-WA0018 (1)_edited.jpg

Charles 

MWEBEYA

Mhariri

Mimi ni mhariri mkuu wa gazeti la Montessori Tanzania ambalo limekuja na mtazamo wa kipekee unaolenga kuisaidia jamii kuondokana na mmomonyoko wa maadili kupitia agenda ya elimu na malezi. Kama mhariri mkuu nitahakikisha makala zinazoandikwa na gazeti hili zinajikita kwenye dhamira kuu ya gazeti kwa kuibua na kuweka agenda katika masuala adhimu yanayoikabili jamii. Makala zitawasilishwa kwako katika kiwango hitajika na misingi ileile ya kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha kwa kutumia lugha rafiki.

IMG_1983_edited.jpg

Elisa Kaimukilwa

KAIMUKILWA

Mwandishi

Nipo Montessori Tanzania kama mwandishi wa makala maalum na pendwa za Dirisha la mzazi na Nuru ya kijana ambazo napenda nikualike ndugu msomaji uweze kuzifuatilia ili upate kilichokusudiwa kwani zinalenga kumkumbusha mzazi wajibu wake katika malezi na maisha yake binafsi. Unapobahatika kusoma makala hizi, usiwe mchoyo mshirikishe na jirani yako ili naye afaidi. Karibu uwe mmoja wa familia yetu kwa kujisajili sasa

bottom of page