Wakulima tulipokee kama neema na siyo kama shuruti
- Anord Jovin
- Aug 6
- 3 min read
Updated: Aug 13
Na Anord Kailembo
Mkoa wa Kagera ni kati ya mikoa Tanzania ambayo inategemea kahawa kama zao kuu la biashara, wakulima walio wengi wamekuwa wakitegemea zao hili kwa ajili ya kujiingizia kipato cha familia.
Inaelezwa kuwa kahawa ya maganda inayozalishwa mkoani humo ni wastani wa tani 50,000 kwa mwaka, thamani ya zao hili imekuwa ikikuwa kila kukicha katika soko la dunia kiasi cha kahawa kilo moja kuuzwa kwa zaidi ya shilingi 5000 msimu uliopita.
Kutokana na ukuaji wa thamani ya zao la kahawa na kuwa na matumizi mengi kwenye uzalishaji wa bidhaa mbalimbali duniani, imewekwa miongozo na sheria ya kulilinda zao hili tangu likiwa shambani hadi linapofika sokoni ili kuwa salama kwa mazingira na watumiaji wa bidhaa zitokanazo na kahawa.
Ipo miongozo ya soko la jumuhiya ya Ulaya inayoelekeza kilimo cha zao la kahawa lifanyike kwa kulinda mazingira, kwa maana ya kwamba miti na mime mingine isikatwe kuondoa kwa ajili ya kupanda kahawa na badala yake inatakiwa kupandwa ndani ya mimea mingine.
Lakini pia ipo sheria ya kahawa namba 23 ya mwaka 2021 na kanuni zake za mwaka 2013 zinaelekeza usimamizi katika utekelezaji wa kilimo cha kahawa, kusajiliwa kwa mashamba sambamba na kuwa kwenye mfumo ili kutambuliwa na kurahisisha mipango.
Katika utekelezaji wa miongozo na sheria za ndani ya nchi na za kimataifa, umeanza utekelezaji wake ikiwemo kubaini mashamba ya zao hilo sambamba na afua ya kuwasimamia.
Tayari wataalam wa ukusanyaji wa taarifa, bodi ya kahawa, watafiti sambamba na serikali wako kwa wakulima wakiendelea na zoezi la kubaini mashamba yanayotumika kwa zao hilo na baada ya zoezi hilo suala la elimu kwa wakulima juu ya uhifadhi wa mazingira kwenye shamba lao uweze kuanza.
Ndugu msomaji hapa nataka tujadili suala la uhifadhi wa mazingira kwenye maeneo ya shughuli za kilimo, imezoeleka katika jamii zetu, mkulima anapotaka kuandaa shamba amekuwa akikata mimea na wakati mwingine kuchoma moto eneo anakotarajia lifanyike shamba.
Hali hiyo imekuwa ikipelekea kila uoto na viumbe vilivyoko kwenye eneo hilo kuteketea moto hali ambayo si sawa kwa mazingira na kwa miumbe wengine ikiwemo binadamu katika upande wa hali ya hewa.
Mazingira uharibika kiasi cha ardhi kumomonyoka lakini viumbe mbalimbali hasa wadudu uteketea huku shida kubwa zaidia imekuwa kwenye mabadiliko ya tabia ya nchi.
Tunaambiwa baadhi ya mambo yamekuwa yakitokea kwenye mfumo wetu wa maisha kutokana na mazingira mfano mzuri ni majira ya mvua, mkoa wa Kagera umekuwa ukipata mvua kwa misimu miwili ya mvua tofauti na maeneo mengine ya tanzania kutokana na uoto wa asili.
Miaka ya hivi karibu majira haya yameanza kupotea, nilipozungumza na afisa mmoja wa mazingira akasema tumeanza kuharibu mazingira kwa kuchoma moto holela na kukata miti.
Ninachotaka kusema ni nini? Ni kwamba tunayo kila sababu ya kila mtu kuyaona mazingira kama ni chanzo kikuu cha ustawi wake baada ya kuwa ameletwa dunani na mwenyezi Mungu.
Kuchukia kila kitu kinachopelekea uharibifu wa mazingira pasipo kusubiri miongozo na s heria za kutubana na kuzitekeleza kwa hofu ya kuwajibishwa na sio thamani kutoka mioyoni mwetu.
Wakulima wa kahawa Kagera wanatakiwa kulipokea hili kama zawadi na siyo shuruti kwani mbali na kuwahakikishia soko la kahawa kwenye mataifa ya ulaya pia inawahakikishia ustawi wa kimazingira na mifumo yake.
Ni vyema watafiti wa wa mbegu za hakawa wakaanza kuzalisha miche ya kahawa inayoendana na mime mingine ili kuwezesha ustawi wa zao hili kuwepo na kutekeleza matakwa ya kisheria na matakwa ya umoja wa ulaya.
Comments