top of page

Tatizo la wanawake kukosa mimba, janga jipya la kiafya

Updated: Apr 17

"Kwa uchunguzi nilioufanya, asilimia kubwa ya tatizo lipo kwa wanaume" Dkt christpher


Na Anord Kailembo


Wakati tukisikia wataalam wa afya wakiyataja magonjwa makubwa na hatari yanayoendelea kuongezeka kwa kasi ikiwomo yakiwemo yasiyoambukiza saratani, shinikizo la damu, kisukari na magonjwa mengine, tatizo la ukosefu wa mimba kwa wanawake ni moja ya tatizo la kiafya linalotajwa kuibuka kwa kasi nchini.


Inaelezwa kuwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya zipo kesi za wanawake kutokupata mimba ile hali wako ndani ya ndoa kwa zaidi ya miaka miwili.


Dkt. Christopher ni daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake kutoka hospitali ya Muhimbili anasema ametembelea hospitali nyingi za wilaya nchini kupitia program ya Samia Suruhu Hassan na kukutana na tatizo hilo.


Anasema baada ya kukutana na changamoto hiyo amebaini kuwa zipo sababu kadhaa zinazochangia tatizo hilo kuibuka kama magonjwa ya zinaa ambayo yanawapata wanawake na kushindwa kupata matibabu mazuri.


“Hapa unakuta mama anapata magonjwa ya zinaa anakwenda kwenye maduka ya dawa pasipo kuwaona madaktari wakamshauri kitaalam hali inayochochea kuziba kwa milija na hivyo kupoteza uwezo wa kumtengeneza mtoto kwa sababu mtoto anatengenezewa kwenye mirija” anasema


Anahitaja sababu nyingine kuwa ni homoni, homoni zinabadilika kulingana na vyakula wanavyokula au kubadilisha mazingira.


Anasema miongoni mwa sababu kuu ambayo inawahusisha wanaume, kuna muda unakuta mwanamke hana tatizo na ndiye ameenda hospitali lakini baba ambaye yawezekana kuwa ndiye mwenye tatizo anashindwa kufika na hivyo kuwa ngumu kuwasaidia.


“Uzazi unategemea baba na mama lakini mara nyingi unakuta wanaokuja hospitali ni akina mama hivyo unashindwa namna ya kumsaidia baba ambaye yawezekana ndiye mwenye tatizo au kuelimishwa pamoja namna ya kila mmoja kufanya yaliyo yake ya kumuwezesha kufanikisha kupata mimba” anasema


Dkt. Christopher anasema kuwa kwa uchunguzi mdogo alioufanya amegundua wanaume ndiyo wenye shida.


Anasema kuwa kuna udhaifu katika utengezwaji wa mbegu ambao unachangiwa na ulaji wa vyakula visivyofaa akitolea mfano zamani watu walikuwa wakila vyakula vya asili sana lakini kwa sasa wanakula vyakula vya kisasa kama chipsi mayai.


“Hii inapelekea utengenezaji wa mbegu unakuwa hafifu lakini pia kuna ambao wanajichua na kufanya mishipa ya mfumo wa uzazi kutanuka pamoja na kunywa pombe na kuvuta sigara kupitiliza” anasema na kuongeza kuwa


“Kwa kawaida mwanaume anapofanya injaculationi moja anatakiwa kuzalisha mbegu si chini ya milioni 25 mpaka 40 na ikiwa chini ya hapo inakuwa na ngumu kumpa mwanamke mimba” anasema Dkt. Christopher


Amesema ametembela hospitali 184 nchi nzima na kila alikokuta changamoto hiyo amekaa na madaktari wa magonjwa ya wanawake na kuwaeleza namna ya kuwasaidia kiafya.


Anawasihi wanando kuwa na Desturi ya kuzifahamu afya zao kwa kufanya vipimo kwa madaktari wa magonjwa husika na kupata ushauri wa namna ya kukabiliana na changamoto ikiwemo eneo hilo la uzazi.

Comments


bottom of page