Moto ni janga linalodhibitika.
- Anord Jovin
- Jun 27
- 3 min read
Na Anord KailemboNa Anord Kailembo
Matukio ya moto ni moja ya majanga yanayowakumba watu, matukio haya yamegawanyika katika Nyanja mbili, yapo matukio yanayowapata watu kwenye nyumba zao lakini yapo yanayowapata kupitia maeneo nje ya nyumba zao.
Matukio ya moto yanayotokea ndani ya nyumba zao ni yale yanayounguza nyumba kutokana na hitilafu ya umeme, mlipuko wa gesi au kuchezea moto wa kawaida; Matukio ya nje ya nyumbani ni yale ambayo hutokea nje ya mazingira ya jengo la nyumba lakini huacha madhara makubwa kwa binadamu na viumbe wengine mfano kuteketeza mbuga na kuharibu mazao, mifugo na kadharika.
Baadhi ya matukio haya hutokea kwa sababu ya kukwepa majukumu katika udhibiti wa moto au umeme, yawezekana ni kutokujali kuhusu maelelezo ya matumizi ya mitungi na mejiko mengine, kutokuchukua taadhali dhidi ya matumizi ya umeme lakini pia imani potofu hasa kwa moto wa nje ya mazingira ya nyumba.
Watu wamekuwa wakipata hasara kubwa kutokana na matukio ya moto ikiwemo kuharibiwa kwa mali na fedha hali inayopelekea mtu kuanza maisha upya na wengine kufirisika kabisa lakini vimeshuhudiwa vifo vya watu kutokana na janga hili..
Mfano hai ni kwamba june 16 mwaka 2025 limetokea tukio la moto wilayani Bukoba mkoani Kagera (kijiji Marehe tarafa Bugabo) la kuteketea kwa nyumba iliyokuwa na wapangaji 16.
Pamoja na mali zilizoteketea moto kwenye nyumba hizo mmoja wa wapangaji alipoteza fedha kiasi cha shilingi milioni 2 alizokuwa amehifadhi kwenye chumba chake cha kulala kama mtaji wa kuanzia maisha.
Inauma, jiulize umejichanga kwa kujinyima ili kufikisha kiasi cha fedha kitakachokusaidia kutimiza ndoto alafu linatokea tukio kama hilo, bila kujali limetokea kwa uzembe au kwa chanzo kisichosahaulika.
Siyo tukio hilo pekee yapo matukio mengi na makubwa zaidi ya hayo ambayo yamesababisha hasara kubwa na kurudisha nyuma ndoto za watu.
Tumekuwa tukisikia kutoka kwenye mamlaka zinazohusika na uchunguzi wa matukio ya moto ikiwemo jeshi la zima moto na uokoaji baada ya uchungu zikiyataja maeneo haya kuwa sehemu ya vyanzo vya matukio ya moto ikiwemo itirafu ya umeme, matumizi ya moto na mripuko wa gesi na muda mwingine hudai kuwa baadhi ya matukio ni kutokuchukuliwa kwa taadhali za moto.
Kila matumizi ya nishati yamekuwa na miiko yake kwa maana ya misingi katika matumizi, mfano tukianza na moto wa kawaida wa kupikia, kutumia kwenye kibatari, koroboi na kadhali tunafahamu kwamba moto wa aina hiyo unatakiwa kuwa mazingira ambayo hautagusa vifaa vyenye kueneza moto kwa haraka mfano nyasi, karatasi au hata mafuta yanayochochea uwakaji wa moto.
Alikadhalika kifaa kama gesi na umeme ipo miiko yake ambayo inaelekezwa na wataalam wa nishati hizo katika matumizi ili kuepuka shida inayoweza kutokea.
Mfano kwenye umeme, mwenye nyumba anapewa kipindi maalum cha kufanya ukarabati wa miundombinu ya umeme lakini kutokana na mazoea ya kuendelea kupata nishati hiyo pasipo changamoto watu hujisahau na mwisho wa siku tukio la kushtukiza la umeme kuripuka hutokea na kuharibu mindombinu ya nyumba, mali na vitu vingine.
Yawezekana wengine tunatumia vitu hivi kwa sababu vipo, tumevikuta katika mazingira yetu hivyo hatukuwahi kujielimisha wala kuona kama kuna umuhimu huo.
Na kujielimisha kuko katika namna nyingi ikiwemo kujisomea kuhusu nishati hizi na masharti yake, kutembelea mamlaka zinazohusika na usimamizi wa nishati ikiwemo jeshi la zima moto pamoja na shirika la ugavi wa nishati ya umeme nchini TANESCO.
Tulio wengi tumekuwa tukijua wajibu huu baada ya kuwa tumepatwa na matatizo, lakini ni wajibu wetu wa msingi kuufanya hata kabla ya kuanza kutumia baadhi ya nishati hasa kubwa kama umeme na gesi ili kuepuka madhara.
Mbali na hilo pia ni wajibu wetu kuheshimu na kutekeleza matakwa ya matumizi ya nishati hizo ambayo hupatiwa pale tunapopewa huduma hizo.
Mbali na hilo pia mamlaka zinazohusika na udhibiti wa huduma za nishati zinao wajibu wa kuhakikisha huduma yao inatolewa kwa ufanisi kwa kuzingatia viwango vya ubora.
Kutoa elimu ya kutosha kwa mhusika kabla ya kuanza kutolewa kwa huduma ili kuijua miiko ya matumizi ya nishati hiyo itakayomuwezesha kuchukua hatua pindi anapobaini viashiria vya hatari katika matumizi ya huduma hiyo.
Kuwepo kwa uhusiano na mawasiliano ya karibu kati ya watoa huduma na wapokea huduma ili hata kuwasiliana kwa pamoja kuboresha huduma.
Iwapo kila mmoja atatimiza wajibu wake (taasisi zinazotoa huduma pamoja na watumiaji wa huduma za nishati) matukio ya moto yanaweza kubaki historia.










Comments