Kijiji kidogo cha wavuvi kilivyogeuka lulu Duniani
- Charles Mwebeya
- Mar 21
- 5 min read
Updated: Apr 17
Na Charles Mwebeya
Wanasema usicheze na zama, zama zinabadilika.. Miaka ya 1960 hadi katikati ya 1980, ndoto za vijana wengi ilikuwa ni kuzamia meli kwenda Ugiriki ama kuibukia Italy ili kutafuta njia nyingine za kusaka maisha .
Hawa nao zama zao ziliishia katika miaka ya 1990 njozi za vijana zilipohamia kughushi nyaraka mbalimbali ili kujaribu kwenda Marekani huko ndipo yale majani mabichi ya mafanikio yalipodaiwa kupatikana.(Green pastures).
Nakumbuka nami nilijaribu kwenda katika ubalozi wa Marekani kipindi hicho walau kujaribu bahati yangu lakini niliangukia pua kutokana na masharti lukuki niliyopewa ambayo sikuweza kuyamudu.
Nilijidai eti nataka kwenda Marekani kwa ajili ya masomo ili baadaye nikibahatisha niingie zangu mitini,,, ndivyo wengi walivyokuwa wakifanya; Miaka hiyo ya 1990 hakuna ubalozi uliokuwa ukifurika vijana waomba viza kama ubalozi wa Marekani.
Wengi waliojaribu kwa mara ya kwanza walifanikiwa na kuweza kuwavutia waliosalia lakini moja ya masharti yaliyokuwa yakiwashinda wengi ni kuwa na taarifa ya kifedha ya muhusika yaani (Bank statement) ambayo ilikuwa ikihitaji kiasi fulani cha fedha kuwa nacho.
Hawa nao sasa enzi zao zimefikia ukomo.. raha ya dunia sasa imehamia jangwani !!..unajua ni wapi? Wakati wa vita ya kwanza ya dunia 1919, Dubai kilikuwa ni kijiji chenye wakazi wapatao elfu 20 tu, wengi wao wakiwa ni wavuvi waliokuwa wakiitumia Ghuba ya uajemi ambayo kwa sasa inajulikana kama Ghuba ya arabu, kuvua samaki na kujipatia kipato na chakula.
Damu ya biashara kwa watu wa Dubai katika miaka hiyo iliweza kuwavuta watu wengi kutoka katika mataifa ya jirani kama Iran, Pakistani pamoja na India hivyo mara baada ya vita kumalizika Dubai na Abu Dhabi ikatawaliwa na Uingereza pamoja na falme nyingine ndogondogo ikiwemo Ajmani, Sharjah, Fujairah na Khaimah.
Pamoja na kuwapo Waingereza bado falme hii ya Dubai ilikuwa kama makutano ya wafanyabiashara kwani biashara ya vito vya thamani iliibuka kutoka maeneo tofauti na kuletwa hapo na hivyo kuchangia ongezeko la watu siku hadi siku.
Mwaka 1971 nchi hizo za kiarabu zilipata uhuru kwa pamoja na kuungana na kuwa umoja wa falme za kiarabu (UAE) ambapo milki nyingine ya Al Quwain ilikuwa ya mwisho kujiunga na umoja huo mnamo mwaka 1972 na inaelezwa kuwa wakati huo Dubai kulikuwa na ghorofa moja tu!!
Baada ya kugunduliwa kwa mafuta, watu wengi wa Imarati waliacha biashara ya lulu na kuanza biashara katika sekta ya mafuta na walipopata uhuru kutoka kwa Uingereza mnamo 1971, uzalishaji wa mafuta uliongezeka ghafla, kusaidia uchumi wa eneo hilo.
Na Dubai ikawa kitovu cha biashara. Mafuta kwa sasa yanachangia pato la falme hiyo kwa asilimia 6 tu huku ikielezwa kuwa akiba yake ni ndogo mno kuinufaisha nchi hiyo kwa siku za usoni.
Wengi wanajiuliza kama mafuta yamefikia ukomo wake mbona bado Dubai inaendelea kuuteka ulimwengu kiuchumi? Januari 3, 1995 aliyekuwa mtawala wa Dubai Sheikh Maktoum bin Rashid Al Mak toum alimteua mwanaye Sheikh Mohamed bin Rashid Al Maktoum kama mfalme mpya wa Dubai ambaye ndiye makamu wa Rais wa falme zote za kiarabu.
Kwani Rais wa UAE hutokea katika falme kubwa ya Abu Dhabi. Baada ya kuitawala Dubai Maktoum alikuja na maono mapya ya kuifanya Dubai kuendelea kustawi pasipo kutegemea biashara ya mafuta kama zilivyo nchi nyingine za mashariki ya kati.
“Huyu mtu (Maktoum) ameacha alama kubwa katika milki yake, watu wa hapa wanampenda sana kwani amefanya mengi kuibadilisha Dubai” anasema Joseph Luse kelo
Mtanzania anayejishughulisha na masuala ya kibenki huko Dubai. Maktoum ndiye mfalme pekee aliyekuwa na njozi za kutaka Dubai iwe gumzo duniani akitaka milki hiyo ya Imarati iwe na miundombinu ambayo haipatikani sehemu yoyote nyingine ili kuivutia dunia na kuwa sehemu kubwa ya utalii.
Ndipo hapo ujenzi mkubwa wa miundombinu ya barabara, majengo ya kuvutia yalipoanza kuipa sifa Dubai. Kwa sasa barabara za milki hiyo, majengo na kila kitu ni zaidi ya kile unachokiona barani ulaya. Uingereza mnamo 1971, uzalishaji wa mafuta uliongezeka ghafla, kusaidia uchumi wa eneo hilo. Na Dubai ikawa kitovu cha biashara.
Mafuta kwa sasa yanachangia pato la falme hiyo kwa asilimia 6 tu huku ikielezwa kuwa akiba yake ni ndogo mno kuinufaisha nchi hiyo kwa siku za usoni. Wengi wanajiuliza kama mafuta yamefikia ukomo wake mbona bado Dubai inaendelea kuuteka ulimwengu kiuchumi?
Januari 3, 1995 aliyekuwa mtawala wa Dubai Sheikh Maktoum bin Rashid Al Mak toum alimteua mwanae Sheikh Mohamed bin Rashid Al Maktoum kama mfalme mpya wa Dubai ambaye ndiye makamu wa Rais wa falme zote za kiarabu.
Kwani Rais wa UAE hutokea katika falme kubwa ya Abu Dhabi. Baada ya kuitawala Dubai Maktoum alikuja na maono mapya ya kuifanya Dubai kuendelea kustawi pasipo kutegemea biashara ya mafuta kama zilivyo nchi nyingine za mashariki ya kati.
“Huyu mtu (Maktoum) ameacha alama kubwa katika milki yake, watu wa hapa wanampenda sana kwani amefanya mengi kuibadilisha Dubai” anasema Joseph Luse kelo
Mtanzania anayejishughulisha na masuala ya kibenki huko Dubai. Maktoum ndiye mfalme pekee aliyekuwa na njozi za kutaka Dubai iwe gumzo duniani akitaka milki hiyo ya Imarati iwe na miundombinu ambayo haipatikani sehemu yoyote nyingine ili kuivutia dunia na kuwa sehemu kubwa ya utalii.
Ndipo hapo ujenzi mkubwa wa miundombinu ya barabara, majengo ya kuvutia yalipoanza kuipa sifa Dubai. Kwa sasa Milki hiyo iliyoanza kujengwa majengo ya kuvutia toka mwaka 1995 bado haijasimama, hii leo ujenzi wa barabara pamoja na majengo mbalimbali ya kukodisha na mahoteli bado unaendelea huku mengine yakiwa tayari yamekamilika.
Moja ya majengo hayo ni pamoja na Burj Khalifa jengo refu kupita yote duniani ambalo lina urefu wa zaidi ya mita 828 likijengwa kwa muda wa miaka mitano kuanzia 2004 na kukamilika mwaka 2009 kwa gharama ya dola za kimarekani bilioni 1.5.
Ujenzi wa visiwa vinavyofanana na mti wa mtende Jumairah katika maeneo ya Rash diyah nao ukaishajihisha Dubai na kuwa kivutio kikubwa cha utalii duniani. Mauzo ya vito vya thamani ikiwemo almasi, nao ukawa chanzo kingine cha kuwavuta watu mashuhuri kwenda Dubai ingawa madini hayo hayachimbwi nchini humo.
Dubai yenyewe inakadiriwa kuwa na watu zaidi ya milioni 1.3 lakini wenyeji ni asilimia 15 tu na waliobakia ni watu kutoka mataifa mbalimbali zaidi ya 200 ambao wamekwenda kutafuta ajira ama kuwekeza katika sekta mbalimbali nchini humo.
Kwa sasa ndio mahala ambapo hupokea watu wengi kuliko sehemu yoyote duniani. Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2023, Dubai ilipokea zaidi ya wageni milioni 17 katika kipindi cha mwaka mmoja ambao walifika na kuondoka kutokana na shughuli mbalimbali za biashara na utalii.
Uwanja wa ndege wa Dubai ni wa pili kwa kupokea wageni wengi Duniani sambamba na ndege nyingi pia. Kwa mwaka 2009 pekee uliweza kupokea abiria zaidi ya milioni 80 kwa mwaka ukitanguliwa na uwanja wa ndege wa Harts field Jackson wa Marekani.
Wengi wa wageni wanaoitembelea Dubai kwa utalii hutokea barani Ulaya, huku wale wanaokwenda kutafuta ajira hutokea nchi mbalimbali za bara la Asia na Afrika.
“Wanapenda sana kuajiri watu wa Asia kwani hawa jamaa ni wavumilivu na sio rahisi kulalamika, pengine ni kutokana na shida wanazopitia huko kwao” anasema Joseph Warioba Mtanzania anayeishi Dubai.
Kwa sasa fursa nyingi za ajira hutokea Dubai kuliko mataifa yoyote Duniani kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa katika sekta za utalii, biashara za nguo, vito vya thamani ..Teknolojia katika nyanja za fedha na uchumi pamoja na ujenzi wa miundombinu mbalimbali ambao bado hauonyeshi kufikia ukomo.
Kinachovutia wafanyabiashara wengi kuja kuwekeza Dubai ni sera za kodi ambazo zinampendelea mno mwekezaji. “Hapa unaweza kufanya biashara hata miaka 15 bila ya kuulizwa kodi ili mradi tu biashara yako ifuate matakwa mengine ya serikali kwani wanaamini sana katika kumjenga mfanyabiashara kwanza ili waweze kuchukua kodi yao baadaye” anasema Warioba.
Sio siri tena kuwa Dubai kwa sasa imeiteka Ulaya, hakuna mwenye hamu tena ya kuzamia Ulaya wala Marekani kwa kuwa hata wazungu wenyewe kwa sasa wame jazana Dubai wakifanya shughuli mbalim bali zinazowaingizia kipato na kukamilisha ule msemo kuwa ..zama zimebadilika!!.
Comments