Hatari! kuweka vinywaji juani
- Wariyoba Wariyoba
- Mar 29
- 5 min read
Updated: Apr 17
Na Wariyoba Wariyoba, Morogoro
Tanzania ni miongoni mwanchi zenye viwanda vingi vinavyozalisha vinywaji ambavyo vimesaidia kwa kiasi kikubwa kuchochea uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Kuwepo kwa viwanda hivi imekuwa chanzo cha nchi kupata mapato kupitia kodi zinazolipwa na viwanda husika, wananchi kupata ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja bila kusahau kuwezesha upatikanaji wa bidhaa zinazozalishwa.
Wazalishaji na wataalam wa afya wamekuwa wakitoa tahadhari katika uhifadhi na matumizi ya bidhaa husika ili kuleta tija kwa mtumiaji pasipo kumsababishia madhara ya afya.
Vipo baadhi ya vinywaji ambavyo vinahitaji kuhifadhiwa katika maeneo maalum kwa ajili ya kutokupoteza ubora kabla ya muda wake wa kuwa sokoni kumalizika na ndiyo maana uambatana na maelekezo ya namna ya kutumiwa na kuhifadhiwa kwenye kifangashio chake.
Wameshuhudiwa baadhi ya wafanyabiashara wa bidhaa hizi nchini kwenda kinyume na matakwa ya wazalishaji wa vinywaji hivyo sambamba na sheria zinazosimamia usalama wa chakula ambapo baadhi yao huweka vinywaji vyenye kuhitaji ubaridi juani hali inayohatarisha ubora wa bidhaa yenyewe.
Sababu zinazochangia baadhi ya wafanyabiashara hasa warejareja kwenda kinyume na taratibu za uhifadhi kuwa ni pamoja na ukosefu wa elimu ya uhifadhi wa vinywaji na upuuziaji wa taratibu, miongozo na sheria za usalama wa chakula.
Daktari bing wa wa magonjwa ya saratani Hospitali ya Ocean Road Dk. Ernest Magembe anasema kitendo cha kuweka vinywaji juani siyo salama kwa afya ya mlaji au mtumiaji kwa sababu inaweza kuchangia kuwepo kwa saratani.
Anasema kuwa chupa iliyotengenezwa kwa ajili ya kuhifadhi vinywaji au vyakula vya wiwandani hutengenezwa kwa kemikali, hivyo bidhaa husika inatakiwa iwekwe sehemu salama isiyokuwa na hali ya joto ili kuepuka kemikali iliyotumika kutengeneza chupa/kifungashio na iliyopo kwenye bidhaa husika kuto haribika.
“Kitendo hiki ni hatari kwa afya, mamlaka husika hazipaswi kulifumbia macho suala hili kwani kitendo cha kuweka vinywaji vilivyotengenezwa kwa kemikali za viwandani juani kunahatarisha sana usalama wa mtumiaji kiafya”anasema Magembe.
Anasema kitendo cha kuweka bidhaa hizo juani hufanya kemikali zilizotumika kutengeneza kifungashio na hata zile zilizopo ndani ya kinywaji husika kuharibika au kupoteza ubora wake hivyo kuweza kumsababishia madhara mtumiaji ikiwemo matatizo ya satarani.
“Zile kemikali zilizopo kwenye kinywaji ukizihifadhi kinyume na utaratibu uliowekwa kwenye kifungashio na mtengenezaji au mzalishaji inaweza kupelekea kuharibika kwa haraka” anasema Dkt. Magembe
Naye Dkt. Abudi Sangali kutoka Ocean Road anasema kuwa mpaka sasa hakijabainika chanzo halisi cha saratani isipokuwa viashiria vyake na kwamba kitendo cha utumiaji wa viywaji kinaweza kusababisha saratani ya ini, koo pamoja na utumbo.
Anasemba mbali na kemikali pia kuweka vinywaji juani kuna sababisha vinywaji husika kupote za virutubisho vilivyokusudiwa na mtengenezaji.
“Vinywaji hivyo huwa na virutubisho vya vitamini ya aina mbalimbali hivyo kitendo cha kuweka juani husababisha virutubisho kupotea na kuchangia kuwepo kwa viashiria vya saratani kwa wa tumiaji” Anasema Sangali.
Pia ameongeza kuwa vinywaji vikiwekwa juani hupote za radha yake ya asili kwa sababu ya shughuli za kemikali zilizokuwa zimefanyika wakati wa kuandaa bidhaa hiyo, pia kusababisha harufu ambazo hazikutarajiwa.
Anasema kuwa siyo jambo zuri kwa bidhaa za aina yoyote ambayo huliwa kuwekwa juani kwani hutengenezwa viwandani na utengenezaji wake huwa ni wa kemikali mbalimbali ikiwemo rangi hivyo kitendo cha kuweka juani huaribu kemikali hizo na kuwa chanzo cha viashiria vya saratani.
Dkt Sangali ameziomba mamlaka zote zinazohusika na suala hili kuwadhibiti wafanyabiashara wote wanaoweka bidhaa zao hasa za vyakula na vinywaji juani kwa kuzingatia usalama wa chakula kwani bila hivyo taifa litaangamia kwa magonjwa.
TBS
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanza nia(TBS) Dkt. Athuman Ngenya anasema vinywaji vina kemikali mbalimbali za asili na za kuongeza hususani vile vya viwandani ambavyo kemikali huongezwa kwa malengo maalum kama vile kuonge za muda wa matumizi (shelf life).
Anasema kuwa mwanga wa jua ni kichocheo ambacho huweza kupelekea mabadiliko ya kemikali hizo kuwa tofauti na hivyo kuweza kuathiri ubora na usalama wa bidhaa hizo na kusababisha athari za kiafya kwa mtumiaji.
“Aidha kuna uwezekano wa watumiaji wa vinywaji hivyo kukosa virutubisho walivyotarajia kama vile vitamini na madini mbalimbali na hivyo kupata athari za kilishe kama vile magonjwa ya ngozi, uchovu, upungufu wa damu na magonjwa ya mifupa pia bidhaa zilizowekwa juani kwa muda mrefu hupoteza ladha halisi ya vinywaji hivyo”anasema Ngenya.
Dkt. Ngenya anasema uhi fadhi wa bidhaa za chakula unasimamiwa na Sheria ya Viwango, Sura 130 na Kanuni zilizoandaliwa chini ya Sheria hiyo na kwamba kifungu namba 20 (a) cha “The Standards (Registration of Premises and certification of products) Regulations, 2021 kinakataza mtu yeyote kuuza au kutunza chakula katika jengo ambalo halijasajili wa na shirika.
Aidha, kanuni namba 21, 2 (a – i) ya kanuni tajwa inatoa matakwa ya namna ambavyo jengo la kuuzia na kutunzia chakula linapaswa kukaguliwa kabla halijasajiliwa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha jengo linakuwa na nafasi ya kutosha kutunzia bidhaa husika na vilevile, viwango vya bidhaa za chakula husika kuainisha takwa la mzalishaji kueleza namna chakula hicho kinavyotaki wa kuhifadhiwa.
Anasema kuwa endapo mfanyabiashara atakiuka Sheria hiyo na Kanuni zilizo andaliwa chini ya Sheria hiyo anaweza kutozwa na shirika faini ya kiasi cha fedha kisichozidi milioni 20 za kitanzania endapo atakiri kosa.
Lakini pia shauri hilo likifikishwa mahakamani na ikabainika kuwa ni kweli mhusika ametenda kosa hilo anaweza kupewa adhabu ya kifungo kisichopungua mia ka miwili (2) au kutozwa faini kiasi cha fedha za kitanzania kisichopungua milioni hamsini na kisichozidi milioni mia moja au vyote viwili.
“Shirika huwakumbusha mara kwa mara wazalishaji, wasambazaji na wauzaji wa bidhaa za chakula kuhakikisha kuwa bidhaa zote za chakula zinahifadhiwa sehemu sahihi ambayo hakuna jua ambalo linaweza kuathiri bidhaa hizo”anasema Dtk. Ngenya.
Dkt. Ngenya anatoa rai kwa wafanyabiashara wote kuepuka kutunza/kuhifadhi bidhaa za chakula juani kwani madhara yake kiafya ni makubwa na kwamba wahakikishe wanazingatia maelekezo ya mazingira ya kuhifadhi bidhaa hizo kama ambavyo hutolewa na mzalishaji katika vifungashio (lebo).
Ally Machela ni Mkuru genzi Mtendaji Manispaa ya Morogoro anakiri kuwepo kwa changamoto hiyo kwa baadhi ya wafanyabiashra na kwamba idara ya afya na biashara zimekuwa zikitoa elimu na katazo la kuweka bidhaa zao juani.
Anasema halmashauri inao mpango wa kuwachukulia hatua za kisheria baadhi ya wafanyabiashara wanaokaidi matakwa ya sheria kwani kitendo wa kuweka bidhaa juani ni kuhatarisha afya za watanzania na pia ni kinyume cha sheria ya afya namba moja ya mwaka 2009 kifungu cha 142 na 148 inayozuia bidhaa ya vyakula kuwe kwa juani.
Anasema kuwa manis paa hiyo inaendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara hao kuacha kuweka bidhaa za chakula juani ambapo pia amewataka kufanya shughuli zao kwa mujibu wa sheria zilizipo nchini.
Amina Iddi Mshana ni miongoni mwa wafanyabiashara manispaa ya Morogoro anakiri kukiukwa kwa taratibu za uhifadhi wa vinywaji na kutambua madhara anasema hana uwezo wa kuhifadhi bidhaa hiyo kwenye stoo kwani ana mzigo mkubwa na pia gharama za utumiaji wa stoo Morogoro ni kubwa.
Naye Mosha Tito anakiri kuwa uwekaji bidhaa vinywa ji nje siyo salama kwa afya ya binadamu ambapo anaeleza kuwa wafanyabiashara wana fanya makusudi kutozingatia usalama wa chakula kutokana na kuona hawachukuliwi hat ua yoyote ya kisheria na mam laka husika.
Comments