top of page

Ulinzi wa viumbe wa majini upo mikoni mwetu, tuyalinde mazingira yao

Updated: Jul 28


Na Anord Kailembo

Kama ilivyo kwa binadamu huitaji mazingira ili kuishi, ikiwa tofauti basi uhai wake hauwezi kuwepo kabisa, mazingira hayo yanaungwa na vitu mbalimbali kama mimea, maji, ardhi, viumbe wengine n.k.


Mazingira hayo humfanya kupata mahitaji muhimu katika kuufanya uhai wake kuwepo mfano hewa safi, chakula n.k vinavyokamilisha dhana nzima ya ustawi wa binadamu.


Ukiacha binadamu pia viumbe wengine waishio, uhitaji mazingira kutokana na maumbile yao ili kustawi, kila kiumbe kimewekewa mazingira yake ya kuishi kutokana na namna kilivyoumbwa.


Wapo viumbe wanaoishi majini, viumbe hawa kwa namna walivyo ni lazima waishi majini ili uhai wao uwepo, mfano wa viumbe hao ni pamoja na samaki, wanyama kama mamba nk.


Pamoja na maji pia viumbe hawa uhitaji vitu vyote ambavyo hupatikana ndani ya maji ili kufurahia maisha na mazingira hayo yakiharibiwa maisha yao yanakuwa hatarini kwani mazingira ndio chimbuko la uhai wao.


Tangu kale maisha ya mwanadamu na viumbe wa majini yamekuwa yakitegemeana, binadamu akihitaji kitoweo basi hulazimika kwenda majini yaweza kuwa ziwani, baharini au mtoni kuvua samaki lakini viumbe hao wakihitaji uvuvi salama kutoka kwa mwanadamu ili kustawisha maisha ya wanaosalia, na imekuwa hivyo.


Kutokana na mabadiliko ya kimaisha na tamaa za binadamu, binadamu amejikuta ni msaliti wa ushirikiano wa kimazingira kwa viumbe wa majini ambapo zilianza kutumika mbinu zisizo rafiki kumnasa samaki hali inayopelekea kuathiri vizazi vya samaki kwa kuharibu mazingira.


Baadhi ya usaliti ni kutumia njia zisizo rasmi za kuvua samaki hao ikiwemo kutumia mabomu, kutumia mtego hatatishi pamoja na kutumia sumu kuvua.


Tukianza na matumizi ya mabomo ni suala linalokiuka taratibu za kawaida za uvuvi salama kwani kutokana na kuharibu mazalia ya samaki na makazi yao pia uua hadi vifaranga vya samaki ambao wangevuliwa siku au miezi ijayo mbeleni.


Matumizi ya mitengo isiyo salama mfano kokolo huelezwa na wataalam kuwa mitego hiyo hukomba samaki wenye sifa na wasio na sifa ya kuvuliwa, hivyo kupelekea samaki kupungua na wengine kupotea kabisa.


Njia ya matumizi ya sumu kuvua samaki, njia hii inatajwa kuhatarisha ustawi wa viumbe hao kuwa yaweza kupoteza kizazi cha aina fulani ya samaki kwani sumu uua samaki wanaokuwepo bila kujali mkubwa na mdogo.


Mbali na njia hizo kudhuru maisha ya viumbe wa majini pia uhatarisha usalama wa watumiaji mfano matumizi ya sumu kiafya si salama kwa mtumiaji ambapo inaweza kumletea madhara.


Kufanya hivi kwa mwanadamu kunaonesha usaliti wa wazi wa mahusiano kati yake na viumbe hao na laiti kama wangekuwa na uwezo wa kutuonesha hasira walizonazo dhidi yetu tunaowafanya kitoweo kwa njia isiyorafiki basi tungeogopa.


Njia hizi za uvuvi haramu zinatajwa na wataalam kuwa zimepelekea baadhi ya samaki kutoweka kabisa kwenye baadhi ya mazingira ya uvuvi na kubaki historia katika maisha ya wanadamu ya kwamba waliwahi kuwepo samaki wa aina fulani.


Lakini tujiulize kwa nini tunawafanyia hivi viumbe hawa ikiwa wenyewe wamejitoa kwa ajili yetu kuwa mazingira ya ustawi wetu baada ya makuzi ya maisha yao?


Hivi tunajiuliza kama ni sisi wanadamu tungekuwa kunafanyiwa hivi tungefurahi? Hivi kwa nini tusiheshimu mfumo wa maisha tuliopatiwa na muumba lakini pia sheria za uvuvi zilizotengenezwa na serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania na sheria za kimataifa?


Yawezekana ni kiburi cha kujaliwa kuyatawala mazingira na viumbe wengine ndicho kinachomfanya binadamu kutokuheshimu mazingira ya viumbe wengine, lakini tunatakiwa kutambua kwamba hata mazingira ya viumbe hao tukiyaaharibu basi tunakuwa tumeharibu mazingira yetu.


Sekta ya uvuvi na rasilimali maji zinao mchango mkubwa katika nchi ikiwemo kutoa fursa nyingi za kiuchumi kwa wananchi ikiwemo wavuvi wenyewe kuingiza kipato, kuvutia utalii pamoja na uwekezaji katika sekta za utalii na uvuvi.


Tunapotumia njia zisizo rasmi kufanya uvuvi lazima tutambue kuwa tunaathiri uchumi wamwananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla bila kusahau kuwa baruti na sumu zinazotumika kuvua zinachafua maji ambayo baadhi ya wanadamu huyatumia kunywa na kupikia.  


Yatupasa kuyaheshimu mazingira na viumbe wanaotuzunguka ni vyema zikabuniwa njia mbadala za kuwanasa viumbe hao katika njia salama itakayoendeleza mfumo wa mazingira ya malezi ya samaki majini.


Yatupasa kuheshimu sheria, kanuni na taratibu za uvuvi tulizowekewa na mamlaka lakini kuwa mabalozi wazuri wa sheria hizo ili kulinda mazingira na rasilimali hizo, kwa kuwaripoti wote wanaokwenda kinyume na ulinzi wa viumbe hao.


Lakini pia ipo haja ya mamlaka zinazosimamia rasilimali za uvuvi kuhakikisha zinaongeza nguvu ya usimamizi ili kuepusha madhara yatokanayo na uvuvi haramu.

 
 
 

Related Posts

See All
Uvivu- adui wa mafanikio ya vijana

Uvivu ni hali ya ukosefu wa hamasa ya kufanya jambo, kukosa nguvu ya kuanza au kumaliza majukumu, licha ya kuwa na uwezo wa kufanya hivyo. Mara nyingi, tatizo hili huwa si tu kutokufanya kazi, bali pi

 
 
 

Comments


bottom of page