Uko wapi na wao wako wapi? 2
- Anord Jovin
- Jun 5
- 5 min read
Na Mwinjilist Elisa Kaimukilwa
Ndugu msomaji na mfuatiliaji wetu wa gazeti hili karibu tena katika mwendelezo wa makala yetu ya “Uko wapi nao wako wapi” iliyokuijia katika toleo lililopita tukiangazia changamoto ya baadhi ya wazazi kukwepa jukumu lao la malezi na kutupa jukumu hilo kwa walezi, waweza kuwa ni wazazi wao, ndugu au jamaa ambaye wana uhusiano naye vizuri.
Katika toleo la 7 tuliona namna wazazi wanavyoshindwa kutimiza wajibu ambao kimsingi wanatakiwa kuufanya kwa wa toto wao ambao ni malezi laki ni leo hii tunaangazia baadhi ya walezi ambao huomba watoto kuwalea kutoka kwa wazazi wao kwa nia ya kujipatia mahitaji ku toka kwa wazazi na sio suala la kuwalea.
Wazazi kumbuka kuwa ninyi bado mna nguvu na uwezo wa kukimbia huko na kule kwa ajili ya kuwatafutia watoto wenu mbali na hilo ninyi ndio wenye mapenzi ya dhati zaidi kuliko yeyote kwa watoto wenu bila kusahau kuwa ninyi mnawafahamu kwa undani watoto wenu kwa maana ya madhaifu na tabia walizonazo.
Kwa umuhimu huo upo ulazima wa mtoto kuwa chini ya uangalizi wako, natambua kuwa kwa ulimwengu wa sasa yaweze kana kutokana na kugubikwa na majukumu tofauti tofauti mzazi ukashindwa kumudu au kupata muda wa kutosha kusimamia malezi ya watoto wako.
Hapa ndipo utashuhudia baadhi ya wazazi wakiwatumia wadada wa ndani ili wasipokuwepo basi watoto wao wawe chini ya uangalizi wa mtu mzima lakini pia sababu nyingine ni pamoja kile tulichokizungumzia toleo lililopita cha mzazi kuamua kumpeleka mtoto wake kwa walezi ambao waweza kuwa ndugu, jamaa au wazazi wake mwenyewe.
Lakini kutokana na madhira ambayo yamekuwa yakiwapata watoto wengi kutokana na wadada wa ndani kutokuwajali ikiwemo ukatili baadhi ya wazazi wanaona njia salama ya kumlea mtoto pasipo uwepo wao ni ku wapeleka kwa walezi wakiamini kwa sababu ya uhusiano uliopo labda wa kindugu si rahisi mtoto kudhurika.
Sasa hapa ndipo ulipo msingi wa mimi kuja na mwendelezo wa mada hii unapoanzia, kuamini kuwa mtoto wako anaweza kulelewa na walezi wengine pasipo kudhurika au kunyimwa haki zao za msingi.
Ni sahihi kuwa wapo baadhi ya watu ambao wamepati wa jukumu la kuwalea watoto wasio wao au kwa kukuomba wenyewe kulea mtoto au watoto na wakaweza kuwapatia haki za msingi sawa na watoto wao kwa maana kuwasomesha, kuwakuza katika maadili mema hadi kufikia hatua ya kujitegemea.
Licha ya kuwepo kwa watu wenye utu na mapenzi na wa toto wasio wa kwao wapo pia wengine ambao kamwe kumlea mtoto wa ndugu, jamaa, rafiki au hata wa mjukuu wake ni changamoto na hapo nataka ni kwambie kuwa usiamini asilimia mia moja kuwa mwanao anawe za kulelewa na mwenzio akapata stahiki sahihi hata kama upo uwezekano wa kupatiwa.
Tumeshuhudia kwenye jamii zetu wale tuliowapa watoto kutulelea ndio huwatumikisha watoto hao, badala ya mtoto kwenda shule basi yeye ana tumia muda huo kumpa bidhaa za kuuza kutembeza maeneo mbalimbali na wengine hutumia muda wa masomo kwa mtoto kumtuma shambani au kuchunga mifugo.
Na kinachosikitisha zaidi ni kuwa yawezekana mzazi ukawa unatuma mahitaji yote ya msingi kwa ajili ya mwanao lakini hayamfikii na yanatumika kinyume kwa mfano unatuma hela ya kununua madaftari inatumika kwenye matumizi binafsi ya mlezi, hela ya chakula cha lishe inatumika vikoba na matokeo yake ni kumkuta mtoto yuko kinyume na matarajio yako.
Pengine unatarajia kumkuta mtoto ana afya njema kwa sababu umekuwa ukituma hela ya matunzo lakini unakuta yupo na utapiamulo mkali, unatarajia mwanao umkute shuleni lakini unamkuta shambani au mjini akitembeza bidhaa ili kupata pesa ya daftari wakati tayari fedha ya kununua mahitaji ya shule tayari umeituma.
Ninachotaka kukwambia ni kwamba, unatakiwa kufanya utafiti na udadisi wako binafsi juu ya mtu unayehitaji akulelee mtoto kabla ya kuchukua jukumu la kumpatia mtoto huyo ili kuepusha madhara mbalimbali yanayoweza kumpata na kuonekana umeshindwa kutimiza wajibu wako kama mzazi.
Pengine utafiti unaweza kuufanya kwa kuangalia tabia binaf si ya mtu unayetaka kumpelekea mtoto, malezi yake kwa watoto wake, uhusiano wako na yeye, utayari wake na ushauri kuhusu kupewa mtoto na huruka aliyo nayo.
Japo na kukumbusha kuwa kufikia hatua hiyo ya kumpeleka mtoto kwa walezi uwe umejiridhisha vya kutosha kuwa huna namna ya kuishi na watoto wako kutokana na sababu za msingi vinginevyo usalama wa watoto wako uko mikononi mwako na si kwa mwingine.
Mbali na kuongea na wewe mzazi pia nizungumze na wewe mlezi ambaye umekubali jukumu la kumsaidia mwenzako kulea watoto kuwa mtoto wa mwenzako ni wako kwa mantiki hiyo unatakiwa kumjali sawa na unavyowajali wa kwako.
Pili ni vyema unaposhindwa kumudu kuishi naye kutokana na changamoto zako binafsi au changamoto za mtoto unayemlea, ukawashirikishe wazazi kuona namna ya kuzitatua na kumuweka mtoto katika hali ya usalama au ukachukua jukumu la kumrudisha kwao ili kuwa huru na kuepuka madhara zaidi.
Mfano; Ukitumia haki ya mtoto huyu anayokuwa ame tumiwa na wazazi wake kwa ajili ya mambo yake na kum tengenezea mazingira ya kuikosa haki hiyo haina tofauti na dhuruma na kawaida dhuruma huambatana na laana ambayo ni dhambi kwa mwenyezi mungu na ni kosa kisheria.
Mfano mwingine ni pale unapotumia kauli chafu na kumtenda matendo yasiyofaa kwa binadamu kama unyanyasaji na utumikishwaji kwa kigezo cha kutokuwa mtoto wako na kumfanya kusononeka na kujuta muda wote basi unatengeneza tatizo.
Kauli hizi huwaumiza sana watoto maana hawana cha kufanya, nao hawajui makubaliano yao kati ya wazazi na walezi wao, maneno haya huwasikitisha, kuwakatisha tamaa, kuwaathiri kiakili na kisaikorojia.
Hali hii huwachosha watoto na kuanza kuwa na fikra mbalimbali wengine huingiwa na mawazo ya kutoroka kwenda kujitafutia mahitaji yao ya lazi ma kwa njia ambayo wao huio na kuwa itawasaidia mtihani wa malezi waliomo na hatua hiyo inakuwa ni mbaya kwani mtoto anapochukua maamuzi ya kutoroka anakokwenda kunaweza kuwa kubaya zaidi.
Na hata wakitoroka baadhi yao hukosa mwelekeo, hukosa pakwenda, kukosa chakufanya, kukosa pakulala, hao kwa sasa ndio tunaowaitwa watoto wa mitaani au panya road, hao ni watoto ambao baadhi ya wazazi wao bado wako hai.
Ikifika hatua hiyo basi huzaa matokeo mengi ikiwa ni pamoja na mgororo wa mtoto na mlezi, mtoto na mzazi, mzazi wa mtoto na mlezi lakini pia mgogoro wa mzazi, mlezi na wadau wa watoto katika kuitafuta haki yao.
Na hatua hiyo ndipo wazazi huanza kujuta wakijiuliza kwa nini walishindwa kutimiza wajibu wao wa kimalezi na kupitia kujiuliza huko basi uanza upambanishaji wa kilichosababisha na matokeo yaliyopo.
Na walio wengi hujikuta sababu ya kusababisha mtoto wake kulelewa na mlezi ni dhaifu sana kulinganisha na matokeo anayoyashuhudia kwa mtoto kwa sababu anakuwa tayari amekomaa kwenye tabia hasi isiyoweza kubadilika kwa muda huo.
Wahenga walisema samaki mkunje angali mbichi, umri wa utoto ni umri ambao anataki wa kuchungwa, kusimamiwa na kuongozwa kwa ukaribu sana maana vitu hivyo vikikosa katika makuzi huenda ikashuhudiwa tabia mbaya na mwenye jukumu na wajibu huo ni mzazi pekee na inapotokea kuwa kwa mlezi basi iwe ni katika mazingira ambayo hakuna namna labda wazazi wamefariki au wamepata matatizo makubwa yasiyoepukika.
TIMIZA WAJIBU WAKO ILI ATIMIZE NDOTO ZAKE
Comments