top of page

Uhusiano wa nidhamu na taaluma kwa mwanafunzi shuleni.

Updated: Mar 15


Nidhamu na taaluma kwa wanafunzi
Nidhamu na taaluma kwa wanafunzi

Na Mwl. Alex Anatory


Naitwa mwalimu Alex Anatory Joachim ni mwalimu mstaafu wa shule ya msingi ninayofuraha sana kupata nafasi ya kuzungumza na wadau wa elimu kupitia jukwaa hili.

Leo hii ninayo shauku ya kuzungumza na wazazi na walezi kuhusu mahusiano kati ya malezi mazuri kwa mtoto (nidhamu) na ufaulu katika taaluma yake wakati wa masomo darasani.


Niseme malezi ni namna mtu alivyolelewa tangu kuzaliwa kwake hadi hatua ya kujitambua, na msingi huo wa malezi anayokuwa ameyapata ndiyo umuongoza katika maisha yake yote.


Malezi hayo yamegawanyika katika namna mbili yapo malezi chanya na hasi, Malezi hasi ni yale yanayompotosha mtoto kwa maana yasiyoipendeza jamii lakini malezi chanya ni yale yanayokubalika kwa jamii.


Mfano, mtoto tangu kukua kwake akiandaliwa katika misingi ya kuwaheshimu wakubwa kwa wadogo kwa maana ya kuwa na nidhamu basi inawemuwezesha kuwa na tabia nzuri lakini mtoto asiyekemewa juu ya ukahidi tangu akiwa mdogo na kuonesha tabia hiyo kwa jamii basi hiyo ni tabia mbaya.


Kama ilivyo kwa binadamu pia taaluma inahitaji nidhamu, mwanafunzi yeyote anawajibika kuwaheshimu wanaomfundisha lakini pia kuheshimu anachofundishwa.

Hili nimelishuhudia katika maisha yangu ya utumishi, unakutana na mtoto anayo nidhamu ya utii wa ratiba na walimu, ‘anawahi shuleni, anakuwa darasani kwa wakati, anakuwa kwenye maeneo anayotakiwa kuwa kwa wakati sahihi.


Unakuta kila mwalimu anapompatia maelekezo katika kazi za ndani na nje ya ofisi anayatekeleza kwa wakati na kwa usahihi bila kubadilisha au kukosoa chochote mtoto wa aina hii ana utii.


Pia nimekutana na watoto ambao wao huenda kinyume na utaratibu wa shule na viongozi wake, unakuta hawakosi kwenye kesi za wanaochelewa, wasumbufu darasani na nje ya darasa, na wengine wanafikia hatua ya kuonesha hata jeuri kwa mwalimu pale anapopewa maelekezo.


Haya yote yanaanzia katika malezi kama mzazi anakuwa hawezi kumuongoza mtoto wake kutimiza wajibu wake kwa wenzie bila shaka ataenda kinyume na utii na hivyo kuwa changamoto kwa wenzake na wanaompatia elimu.


Ni wajibu wa mzazi kuhakikisha anamjenga mtoto wake kukua katika misingi iliyo nzuri kama ilivyo kwenye kuitunza afya yake tangu akiwa mdogo hali hiyo itamfanya kukua akijua kuwa anatakiwa kuishi vipi na jamii.


Anapokuwa na nidhamu chanya kwa walimu ni dhairi shairi kuwa atakuwa na ustawi chanya wa kitaaluma kwa sababu atakuwa tayari kufuata yote anayoelekezwa na ukiangalia asilimia kubwa ya wanafunzi waoafanya vizuri ni wale wenye nidhamu.


Na kwa sababu mtoto analetwa shuleni akiwa katika umri wa kurekebishika basi na sisi tunakuwa na wajibu wa kurekebisha tabia zisizo nzuri kwa mtoto zinazoweza kumuathiri kitaaluma na kimaisha kwa ujumla.


Kwa hiyo siyo wajibu wa mzazi pekee kurekebisha tabia za mtoto ambaye ni mwanafunzi hata sisi walimu na msingi wa malezi kwa mtoto unaimarizaidi pale ambapo mza, mwalimu na jamii wanashirikiana kumlea.

                               Mtoto wa mzazi pekee ni wa jamii nzima

Comments


bottom of page