top of page

Ni wajibu wetu tuukubali

Updated: Apr 16


Naitwa Arobogast Mtayoba ni mwalimu mstaafu tangu mwaka 2019 akiwa katika shule ya msingi Kikukwe kata Kanyigo wilaya ya Missenyi mkoani Kagera nikihudumu kwa zaidi ya miaka 37 katika nafasi hiyo kwenye shule mbalimbali za msingi.


Leo katika kipengele cha asemavyo mwalimu naomba kutoa uzoefu wangu katika eneo la umuhimu wa chakula kwa wanafunzi wa shule za msingi, kama kila mmoja anavyofanyamu usiposhiba basi huwezi kutekeleza kwa ufanisi shughuli zako.


Hii ni kwa sababu chakula kinauongezea mwili nishati ya nguvu ili kuwa tayari kukabiliana na shughuli unayojigusisha nayo, kama ilivyo kwa mtu yeyote ndivyo ilivyo kwa mwanafunzi ili aweze kusoma ni lazima awe ameshiba ili mwili na akili vipate utuliwa wa kupokea anachofundishwa.


Hili nimelishuhudia darasani mwanafunzi ambaye anajifunza bila kula chochote utulivu na umakini wake katika kufuatilia anachofndishwa na mwalimu huwa ni mdogo mno ukilinganisha na Yule ambaye ameshiba.


Yule ambaye hajala yawezekana akapatwa na usingizi wakati wa masomo, kuonesha kutokuwa na utayari wa kumsikiliza mwalimu lakini pia muda mwingi kutokuwa sehemu kabisa ya darasa.


Hata kwenye upande wa taaluma mara nyingi watoto wanaopata chakula wamekuwa wakifanya vizuri kitaaluma kuliko wasiopata chakula, simaanishi kwamba wasiopata chakula hawafaulu la asha, wapo wenye uwezo binafsi yaani wenye akili za kuzaliwa.


Lengo la serikali kuleta mpango wa chakula shuleni ililenga kuwasaidia wanafunzi wote kunufaika sawa kwenye taaluma inayotolewa shuleni, lakini changamoto niliyobaini ni mapokeao ya watekelezaji ambao ni wazazi na walezi.


Baadhi yao wamekuwa wakisimama na kauli ya kuwa “sisi tulisoma bila kupata chakula shuleni mbona tulifaulu” nataka nikuambie kuna mabadiliko makubwa katika ujifunzaji na ufundishaji kwa mwanafunzi.


Kuna suala la ongezeko la muda na vipindi vya masomo, mabadiliko ya mfumo wa maisha, ustahimilivu wa kimwili na kiakili kwa wanafunzi wa sasa na zamani hivyo kusababisha hata namna ya utafutaji wa taalum kubadilika.

 

Lakini changamoto hiyo inachagizwa zaidi na kukosekana kwa ushirikiano baina ya wazazi na walimu ambao ndio waangalizi wa mtoto huyu na hata ilifikia wakati wazazi wanaochanga chakula wanashindwa kuwaamini walimu nakuwahusisha kwenye upotevu wa chakula wanachochanga.


Na kuleta mabadiliko ya sasa wasimamizi wa chakula shulezi chini ya kamati ya wzazi na walimu watekeleze jukumu lao la kitaalum, ukiona ushirikiano wa pamoja kati ya walimu na wazazi unafikia huko basi ujue ufanisi utakuwa duni.


Mimi binafsi kwa uzoefu wangu wa kufundisha wanafunzi nishauri kuwa ili tufikie ufanisi wa taaluma kwa wanafunzi wetu ni lazima kama wazazi tukubali kutimiza wajibu wate wa kuhakikisha chakula kwa ajili ya mtoto awapo shuleni kinapatikana.


Wazazi wenyewe wanaweza kutafuta mfumo mzuri utakaomuwezesha kila mmoja kuweza kuchangia, ili litasaidia kuondoa matabaka yanayokuwepo baina yao yaani wanaopata huduma ya chakula na wanaokosa.


Pili huduma hii kwa sababu unafanyika shuleni na walimu ndio wanaobeba jukumu la usalama wa mwanafunzi awapo shuleni shughuli hii ingewashirikisha wote kwa pamoja maana kama mwalimu hatashiriki basi kuna uwezekano wa kutokupata huduma bora.

“Ni wajibu wetu tuukubali”

Comentarii


bottom of page