top of page

Sala, Uminifu na Upendo.

Updated: Jun 27

Mfahamu askofu Jovitus Mwijage wa jimbo la Bukoba

Na AnordKailembo


Ilikuwa Desemba 12 mwaka 1966 ndipo familia ya Bw, FransisNdibalemana Bi,FransinsikaKokuongeza ilipompata mtoto wao Jovitus Frasins Mwijage, mzaliwa wa parokia ya Ishozi jimbo katoriki la Bukoba katika kitongoji cha Kanyange kijiji Katorerwa kata Ishozi wilayani missenyi mkoani Kagera.


Alianza shule ya msingi mwaka 1976 katika shule ya msingi Kyelima akiwa darasa la sita mwaka 1981 alihamia Rutabo seminari na mwaka 1982 akahitimu darasa la saba.


Alipata elimu ya sekondari katika seminari ya mtakatifu Maria ya Rubya mwaka 1983 na kuhitimu kidato cha nne mwaka 1986, aliendelea na kidato cha tano mwaka 1987akichukua masomo ya kishwahili, Jeografia na Historia (HGK) akiongeza somo la siasa na Hisabati na kuhitimu elimu ya kidato cha 6 mwaka 1989 katika sekondari ya Rubya.


Alipohitimu kidato cha 6 aliteuliwa na aliyekuwa askofu wa jimbo katoriki la Bukoba Nestory Timanywa kufundisha katika shule ya seminari ndogo ya maandalizi ya mtakatifu ya Yohane Bosco ya Rutabo mwaka 1989 hadi mwaka 1990, alijiunga na seminari kuu ya Ntungamo na baadae kwenda seminari kuu ya Segerea Dar es salaam.


Mwaka 1997 alipata digrii ya kwanza ya Teolojia akiwa na ufaulu wa daraja la kwanza.

Alipata daraja la upadre julai 20 mwaka 1997 na kasha kuteuliwa kuwa paroko msaidizi wa parokia ya Mwemage jimbo katoriki la Bukoba kwa mwaka mmoja na baadae alienda seminari ndogo  ya Rubya kuwa mwalimu wa masomo ya jeografia, historia na uraia kwa madarasa ya (o – level na high leve).


Mwezi June mwaka 2005 alitumwa masomoni Roma kusomea historia ya kanisa katika chuo cha kipapa cha Mtakatifu Geregori kuanzia shahada ya kwanza mpaka shahada ya uzamivu (phd) alihitimu mwezi februari 2012.


Wakati akiwa masomoni Roma alipata kwenda kuhudumu katika nchi ya Ujerumani na Austria kama paroko msaidizi.


Baada ya hapo alirejea jimboni kuwa mwalimu wa seminari kuu ya segerea, na baadae kuteuliwa kuwa mkurugenzi wa mashirika ya kipapa nchini Tanzania 2012 kazi iliyodumu nayo hadi mwaka 2023.


Pamoja amekuwa akihudumu kama katibu mtendaji wa umoja wa mapadre wa jimbo Tanzania na katibu mtendaji wa bodi ya seminari kuu (Ntungamo, Kibosho, Kipalapala, Segerea na mwendakulima).


Baada ya hapo alirejea jimbo katoriki la Bukoba kuwa paroko msaidizi wa parokia ya Rwamishenye na ndipo taarifa ya uteuzi wa kuwa askofu wa jimbo la Bukoba ilipomkuta.

Ameiambia Montessori Tanzania kuwa, padre Jovitus anasema alishangazwa na taarifa hizo kwani hakutarajia kama angeteuliwa kushika nafasi hiyo kubwa ya kitume katika jimbo la Bukoba.


Anaamini mwenyezi Mungu ndiye aliyewezesha kuteuliwa na ndiye atakaye muongoza katika kutekeleza utume wake na kwamba katika utume huo atahakikisha anamtanguliza mwenyezi Mungu kwa sala, uaminifu na upendo.


Yanakumbukwa maneno yake wakati akipatiwa daraja la upadre “Mwenyezi mungu ndiye atakayenisimamia, naamini diye aliyeniteua na ndiye atakayenisimamia" Askofu Mwijage


Kabla ya kuwa askofu wa jimbo Katoriki la Bukoba, Padre Jovitus Frasis Mwijage amefanya mambo mengi katika jamii ya kuondoa changamoto zilizopo zinazokwamisha maendeleo kwenye jamii.


Ameweza kujenga shule ya msingi na sekondari ya Moyo mtakatifu wa  Yesu zilizoko jimbo katoriki la Bukoba wilayani Missenyi akidai kuwa alifanya hivyo baada ya kuona wazazi wakiangaika kuwapeleka watoto wao nchi jirani ya Uganda kutafuta elimu nzuri lakini pia wengine wakiishia kutokupata elimu yenye kuwajengea msingi imara wamaisha.


Anasema anaamini ujinga unafutwa na elimu na kwamba ndio maana wamissionari waliamini katika elimu na walifanikiwa kupata elimu yao walifanikiwa katika maisha yao.


Anaamini elimu katika ngazi ya jamii itainuliwa na kuboreshwa na wazawa pasipo kuwasubiri wahisani kutoka nje ya nchi na kwamba ujinga ndicho chanzo cha kukwama kwa ndoto za maisha ya watu wenyewe.


Pia ameandika vitabu mbalimbali na moja ya kitabu hivyo kinatumika kwenye shule nyingi za sekondari chenye jina la MAJOR EVENTS IN AFRICAN HISTORY ambacho anaamini wanafunzi wamepata maarifa na kuchangia kufikiwa kwa ndoto zao.


Askofu mteule Jovitus Fransis amepatiwa daraja la uaskofu januari 27 mwaka 2024.


Akizungumzia utendaji kazi wa wa askofu Jovitus Mwijage aliyekuwa askofu msaidizi na msimamizi wa kitume wa jimbo katoriki la Bukoba ambaye alikabidhi kijiti cha uaskofu kwa Askofu Mwijage, amesema kuwa askofu mwijage ni kati ya mapadre ambao wameyaishi maisha yao kwa kujitoa na kwa uaminifu.


Amesema kuwa katika nafasi zote alizopatiwa tangu akiwa padre amezitekeleza kwa ufanisi mkubwa na kila alipokuwa akitoka sehemu moja kwenda nyingine amekuwa akisifika kwa utume mwema.


“Na mimi nilimtarajia kuwa anaweza akawamiongoni mwa wanaoweza kuteuliwa kuwa askofu wa jimbo la Bukoba licha ya kuwa na mapadre 173 wa jimbo kwa kipindi hicho na wengi wenye uwezo na hii ni kulingana na uwezo mkubwa alionao” alisema askofu kilaini.


Anasema kilichomfurahisha zaidi ni kuwa kipindi hicho anateuliwa ilikuwa ni zaidi ya miaka 40 imepita tangu uteuzi wa askofu ufanyike kwa padre aliyendani ya jimbo lenyewe na kwa mara ya mwisho ilifanyika kwa askofu askofu Nestory Timanywa aliyekuwa askofu wa jimbo la Bukoba.


Histori ya Askofu Mwijage inatufundisha mengi ya kitume lakini pia maisha ya nje ya utume wake, katika utume tunaambiwa alimtanguliza menyezi Mungu katika kila jambo na kila lililotokea katika maisha yake aliamini ni mpango wa Mungu, hii kwetu sisi inatakiwa kuwa somo kwani ukimuweka mwenyezi Mungu mbele hutofanya lililochukizo kwa Mungu mwenyewe pamoja na wanadamu.


Pili tumsikia sifa yake kutoka kwa askofu msataafu Methodius Kilaini kuwa alikuwa mchapakazi kila sehemu alikopelekwa, hii inatufunza uadilifu na kutekeleza vyema majukumu ya kikazi na kimaisha tunayokabidhiwa ili kuitengeneza historia nzuri ya maisha yetu kule tunakotoka na tunakokwenda.


Jambo la tatu ni kuwa wavuvilivu licha ya kuwa na nafasi kubwa za kitume nchini na nje ya nchi hakusita kurejea katika parokia na kuwa paroko, hakuuvaa ule ukubwa aliokuwa nao, hii inatufunza kwamba yawezekana ulikuwa mpango wa Mungu kumpima imani yake ili kumuandalia njia ya kuupata uaskofu, hivyo tusisite kukubaliana na mazingira yawezekana ukawa ni mpango wa mungu kuona uvumilivu wako.

Comments


bottom of page