Ni fahari yetu kuona mabadiliko, fukwe za Bukoba mjini.
- Anord Jovin
- Oct 10
- 2 min read
Miezi kadhaa iliyopitia Montessori Tanzania iliandika makala maalum kuhusu uchafuzi wa fukwe za ziwa victoria ikionesha hasara za kuchafuka kwa fukwe hizo kiuchumi, kijamii na hata kiafya makala iliyopewa jina la Fukwe tiba ya msongo wa mawazo.
Makala hiyo ilifanya uchambuzi kwa fukwe hizo kwa kuzilinganisha na fukwe nyingine ambazo zimekuwa zikifanya vizuri kutokana na kuwa na mazingira mazuri ikiwemo kuwa safi hivyo kumuhakikishia usalama mtu au mtalii anayezitembelea.
Na mara kadhaa watu bila kujali gharama zinazotumika wamekuwa wakisafiri kuziendea ili kupata faraja na mapumziko kwenye fukwe hizo mfano ni Kabuhara beach ambayo iko nje ya mji wa Bukoba lakini watu wamekuwa wakiifuata ili kunufaika na mazingira yake.
Hatua zimechukuliwa ambapo fukwe na mazingira yanayozizunguka yamefanyiwa usafi ikiwemo kufyekwa kwa vichaka, kuondolewa kwa taka ngumu na nyepesi lakini pia kuongezewa thamani kwa kuwekewa miundombinu na vifaa vya michezo na uhifadhi wa mazingira.
Kongole kwa halmashauri ya Bukoba na mkoa wa Kagera kwa ujumla hasa idara za michezo, afya na mazingira kwa jithada zenu za usimamizi wa mambo yote haya hakika kama Montessori ni fahari kubwa sana kwetu kuona matamanio yetu yanafikiwa.
Tumeshuhudia wakazi wa ndani na nje ya Bukoba wakizitumia fukwe hizo katika matumizi mbalimbali kwa siku za kawaida tofauti na ilivyozoeleka siku za jumamosi na jumapili, wameshuhudiwa wakifanya mazoezi, matembezi ya kawaida, mapumziko pamoja na wajasiliamali kutembeza bidhaa zao.
Chini ni baadhi ya matukio ya picha ya kile kinachoendelea sambamba na mwonekano mpya wa fukwe za Bukoba.
Baadhi ya wakazi wa wilaya ya Bukoba wakifanya mazoezi kwenye fukwe za ziwa victoria
Baadhi ya raia wa kigeni wakitembelea fukwe za ziwa victoria na kufurahia mazingira yake kwa kufanya matembezi.
Baadhi ya watu (familia) ambao wamefika katika fukwe za ziwa victoria Bukoba mjini kwa matembezi na mapumziko.














Comments