top of page

Nguvu ya kuanza sasa, leo ina nguvu, kesho ni matarajio

Kuna maneno mawili rahisi ambayo mara nyingi huamua hatima ya kijana: “Leo” na “Kesho.”


Katika maisha ya kila siku, vijana wengi hutumia neno kesho kama kimbilio la muda mahali pa kukimbiza ndoto zao, mipango yao, na matamanio yao.


Wanasema, “Nitafanya kesho, nitaanza kesho, nitaandika kesho, nitaanzisha biashara kesho…” Bila kufahamu kwamba kesho hiyo haijawahi kuja kama walivyodhani.


Ukweli ambao mara nyingi hupuuzwa ni kwamba hakuna aliyepewa hakikisho la kesho, wakati pekee tunaoumiliki kabisa ni SASA.


Katika makala hii, tutachambua kwa undani kwa nini kijana hapaswi kungoja kesho ili aanze kujenga kesho yake, na jinsi tabia ya kusubiri inavyogeuka kuwa mtego wa muda unaowaumiza wengi bila wao kutambua.


Watu wazima wengi ambao leo wana miaka 40 au 50 hukiri jambo moja la kuumiza: “Kama ningejua, ningeanaza mapema.” Usikika wakisema


Hawajui walipoteza lini nguvu, muda, na uimara wa ujana, hawakugundua taratibu jinsi maisha yalivyokuwa yanawavuta katika majukumu mapya ya familia, kazi, gharama, changamoto za kiafya mpaka wakajikuta hawana tena nafasi ya kufanya yale waliyoahirisha wakiwa vijana.


Hii ndiyo picha halisi inayowangoja vijana wanaosema “bado nina muda.”Ukweli ni kwamba muda haujawahi kuwa rafiki wa anayesubiri.


Kila siku inayopita bila kuanza, inakuwa hasara ya kujijenga mwenyewe, kila saa inayopita bila hatua, inakuwa nafasi iliyopotea isiyoweza kurudi, zipo sababu zinazowafanya vijana wengi kuhairisha.


Hofu ya kushindwa, kushindwa si jambo linalowapenda vijana wengi, kuna hofu ya kuchekwa, kuhukumiwa, kutokubalika au kudharauliwa, wengi huvuta muda wakiamini wataanza pale watakapokuwa "wakamilifu." lakini ukweli ni kwamba hakuna aliyefanikiwa bila kushindwa, na hakuna ukamilifu kabla ya mwanzo.


Hii ndiyo sababu kubwa inayowarudisha nyuma wengi. Kushindwa si jambo linalopendwa, hususan na vijana wanaohofia kuchekwa, kuhukumiwa, kutokubalika na kudharuliwa, wengi huamini wataanza pale watakapokuwa “wakamilifu.” Lakini ukweli kwamba hakuna ukamilifu kabla ya mwanzo. Kila aliyejaribu kufanikiwa alikutana kwanza na kushindwa mara nyingi.


Kupungua kwa kujiamini, vijana wengi hujiona hawajakomaa vya kutosha kuanza, wanajilinganisha na waliofanikiwa na kuamini hawawezi kufika mbali, hawajui kuwa hata hao waliowazidi leo walianza mahali ambapo wao wapo sasa.


Mtego wa starehe na uvivu mpole, mazoea ya kuahirisha mitandao ya kijamii, vishawishi vya marafiki, starehe zisizoisha huiba muda polepole, vijana hawatambui kuwa wanatengeneza tabia ya kusubiri bila mipango.


Leo ndiyo kesho unayoitaka, nguvu ya sasa ndiyo msingi wa mafanikio ya baadaye, kesho haitabiriki, haina dhamana, na kamwe haijawahi kuwa ahadi.


Kwa kijana wa leo, hatua ndogo ya leo ina thamani kubwa kuliko mpango mkubwa wa kesho, leo ina nguvu, kesho ni matarajio na maisha hubadilishwa na wanaothubutu kuanza sasa.

 
 
 

Comments


bottom of page