top of page

Ndoa yako inawezaje kudumu

Na Aminiel Uiso

Ndugu mfuatiliaji wa kipengele hiki cha Nuru ya kijana nikukaribishea katika makala ya ndoa yako inawezaje kudumu ikiwa awamu ya kwanza ya makala hii ilikujia katika matoleo yaliyopita ambapo tuliangazia mambo baadhi yanayoweza kui fanya ndoa yako kudumu.


Staha katika ndoa

Staha ni tendo la heshima linaloabatana na haya au aibu ya kutenda jambo lisilo zuri mbele ya watu wengine. Staha ni heshima, hadhi, adabu, na nidhamu.


Staha ni nguzo nyingine muhimu ya kuifanya ndoa kuwa yenye furaha na kudumu, wana ndoa hawana budi kuishi kwa staha kwa kupeana hadhi, heshima na kutendeana mambo kwa adabu na heshima, mke lazima awe na staha kwa mume na mume kwa mke vivyo hivyo.


Nguzo hii ya staha kwa wenzi huwasaidia kuwaimarisha na kuwafanya wenzi wa ndoa kila mmoja aone umuhimu wa na fasi ya mwenzake katika maisha yake.


Katika nyakati za leo, tumeshuhudia wenzi wengi wa ndoa hawatendeani mambo kwa staha, vijana wengi wanajikuta wameingia katika ndoa ila hawaheshimiani, na changamoto kubwa ya wanandoa kukoseana adabu ni kutokana na hadhi za kifedha, elimu au cheo.


Katika enzi za wazazi na wa zee wetu walipokuwa wameingia katika ndoa hakuna aliyekua anaacha kumweshimu mwen zake. “Enzi zetu haikua ajabu unamkuta mtu msomi amemuoa mwanamke wa kawaida wenye elimu ya chini ama mtu tajiri amemwoa mwanamke maskini wa kawaida na siku zote ukikutana nao walikuwa wanaendana na kuheshimiana”.


Hali hii ipo tofauti kwa vija na wa kileo, wanatanguliza elimu zao, fedha, kazi ama vyeo vyao mbele katika mahusiano yao ya ndoa, mathalani utakuta mke anafanya kazi yenye hadhi na kipato kikubwa kuliko mume, wengi utakuta wanaleta dharau kwa wenzi wao, wanajipangia, wanajiamulia na hawawajibiki katika nafasi zao.


Wakati naandaa Makala hii ya sehemu ya pili ya Ndoa yako in awezaje kudumu, Nilikutana na Wanawake wawili wanasimuli ana kwa masikitiko jinsi ndoa ya rafiki yao mmoja iliyofungwa kifahari na namna walivyojitolea kwa furaha kufanikisha ndoa ya mwenzao ila ndoa hiyo haikudu mu zaidi ya miezi sita.


Nilidadisi sababu ya kuvunji ka ndoa hii ni nini, walinijulisha kuwa wanandoa hao wote wali kua wasomi na wanakazi zao na baada ya ndoa kila mmoja aliendelea na kazi yake, wanaamka asubuhi na kurudi jioni.


Na tatizo lilianzia hapo, wakati wanarudi nyumbani jioni, mke hakutaka kujishughulisha na kuandaa chakula, na mume alipomuuliza alimjibu kwa kumkosea adabu na heshima kwamba anamuulizaje habari za kupika chakula wakati wote wa metoka kazini? Mume aliendelea kumsisitiza mke wake juu ya wajibu wake, chaajabu mwanamke yakamshinda akaona bora arudi kwao, hivyo ukawa mwisho wa ndoa hiyo.


Staha ni muhimu sana ya kufanya ndoa iwe yenye furaha na ya kudumu, staha husaidia kuondoa ubinafsi bali kuanga lia maslai ya mwenzi wako, pia staha husaidia wenza wa ndoa kuweza kuishi ingawa wanawe za kuwa na tofauti za mambo mbalimbali, mitazamo ama to fauti juu ya jambo fulani kwa kuzingatia kuwa mke na mume sio kila kitu kitakuwa sawa sawa ama kufanana wakati wote.


Mke aweza kuwa timu ya Yanga na Mume akawa timu ya Simba ila wote wakaishi kwa furaha hata kama timu moja wapo ikifungwa.


Kuwa na staha kwa wenzi wa ndoa husaidia sana kuepusha wanandoa kukoseana heshima hadharani ama faraghani, hata kama mume apaswa kuwa kiongozi wa familia yaani baba, kama desturi zetu zilivyo, ila kuwa baba hakutamfanya awe mbabe, mkorofi, mnyanyasaji, jeuri bali mume anapaswa kuwa kielelezo, mwenye hekima, mnyenyekevu, mwenye huruma na anayemjali mke na watoto bila kusahau wa jibu wake mkubwa wa kuisima mia familia.


Staha pia itamsaidia mke asi mame kwenye wajibu wake na kumsaidia mume wake atimize vyema wajibu wake sio kuingil ia wajibu ama kumwacha mume atelekeze wajibu wake kwa mke yaani mke ndio awe kiongozi wa familia ili hali baba yupo, jambo hili sio staha, ingawa kwa Dunia ya sasa wanandoa wengi haswa vijana wanaongia katika mahu siano ya ndoa wanaonekana kila mmoja hana staha kwa mwen zake, na hii huibua ushindani wa kiupinzani usio na mashiko.


Maneno Matakatifu yanasema “Je Watu wawili waweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana?” Hii haimaani shi kwamba kwa kuwa mume ndio kiongozi wa familia, mke anapaswa kukubaliana na kila kitu bila kuwa mshauri msaidizi na wakati mwingine hata kama hakubaliani anapaswa kutumia staha sio kumkebehi, kumkejeri mume ama kujifanya mjuaji, mwanamke kwa upande wake akiwa na staha itasaidia mume naye kuwa na upendo na staha.


Matokeo ya kuwa na staha kwa wenzi wa ndoa itasaidia sana wanandoa kuwa na mawasiliano mema na mawasiliano ndio nyenzo muhimu sana katika kufanya mahusiano ya ndoa kuwa thabiti lakini staha husaidia kutokubaliana kimawazo kwa wana ndoa isiwe changamoto, kwa kuwa katika staha mawasiliano ya wenzi wa ndoa itakuwa na lugha nzuri ya upole, yakutia moyo na kila mmoja atajisikia faraja na msaada kwa mwenzake nyakati zote.


Kwa ujumla staha huwasaid ia wenzi wa ndoa kusuluhisha tofauti zao kwa njia bora za upole bila malumbano na kufika mwisho mwema kwa kuwa kila mmoja ataheshimu maoni ya mwenzake pia atatambua nafasi na wajibu wake katika hiyo ndoa na kuepuka kuwa king’ang’anizi ama kulazimisha maoni yake mwenyewe kwa ubabe.


Namalizia Makala hii kwa simulizi ndogo wa wazee wawili niliowatembelea siku moja, nilishangazwa sana nilivyokutana na vikongwe hao waliokuwa na upendo na staha ya ajabu.

Jiko la gesi la bibi huyu ambalo alikua analitumia kwa ajili ya kuandaa chakula chao liliharibika, fundi akaja na kuliona jiko hilo akiwa na bibi jikoni, babu alikuwa nje anapunga upepo.


Fundi alipomwambia bibi gharama za matengezo ya jiko, bibi akatoka nje, kumjuza babu alichoelekezwa na fundi, kisha wote wakaenda kule jikoni wa lipomwacha fundi na babu naye akahitaji maelezo na baada ya kupewa maelezo akakubaliana na ile kazi ya jiko kutengenezwa.


Swali kubwa nilililojiuliza, Je ilikuwa na ulazima gani bibi aende kumwambia babu mambo ya jiko (jikoni) wakati lile suala alikuwa anaweza kulimaliza mwenyewe? Jibu nililopata kwamba ndoa hii ya babu na bibi ilikuwa na upendo na staha.


Swali kwa upande wetu sisi vijana wa leo Je, ndoa zetu tu mezisimamisha katika nguzo gani ili ziwe na furaha na kudumu?

 
 
 

Comentarios


bottom of page