Nafasi ya michezo katika masomo shuleni
- Anord Jovin
- May 9
- 1 min read
Updated: 3 days ago
Naitwa Enelietha Emmanuel mwalimu katika kituo cha Tegemeo Montessori Manipaa ya Bukoba mkoani Kagera nimekuwa tegemeo kwa miaka miwili sasa nikifundisha wanafunzi wa madarasa ya awali.
Leo hii nataka kuzungumzia umuhimu wa michezo katika ufundishaji kwa mwanafunzi, suala la michezo lina tija sana kwa mwalimu na mwanafunzi.
Michezo imegawanyika katika namna tofauti ipo michezo ya watoto wenyewe na ipo michezo inayotumiwa na walimu kama sehemu ya kufundisha tofauti na kukaa darasani.
Michezo ya wanafunzi wenyewe ni ile ambayo unakuta wanafunzi wanafanya kwa ajili ya kujiburudisha au kufurahi mfano mpira wa miguu, kukimbia na kucheza mziki hii huwasaidia kuchangamsha mwili na akili na kuwaweka tayari kupokea kile ambacho wanafundishwa darasani.
Lakini pia ipo michezo ya kimasomo ambayo mwalimu badala ya kuingia darasani na wanafunzi basi analazimika kwenda sehemu nyingine yenye mazingira rafiki kwa mchezo husika na kuamua kuwashirikisha wanafunzi katika mchezo huo ili kufikisha kile ambacho anakilenga kwa anaowafundisha.
Lakini pia tusisahau kuwa michezo mingine yaweza kufanyika madarasani kwa maana ya mazingira ya darasa.
Sisi hapa shuleni tunayo michezo rafiki kwa masomo na watoto mfano ukazo wa fikra, huu ni mchezo unaomfanya mtoto kuwa makini pale anapokuwa anasikiliza au kuandika, mchezo mwingine ni mchezo wa kumbukumbu humsaidia mtoto kuwa makini na kukumbuka mwenzake alichokitenda.
Na hii haimaanishi michezo mingine ya watoto wenyewe kuburudika hatuna la asha! tunavyo viwanja na vifaa kwa ajili ya michezo mbalimba kama mpira wa miguu, mikono, kumbembea, kuruka kamba pamoja na kuteleza.
Nawashauri walimu wenzangu hasa wa madarasa ya chini kuwa michezo inasaidia katika kumfanya mwanafunzi elewe zaidi hivyo wawe wabunifu katika kutafuta michezo itakayowasaidia kuwasilisha somo kwa uweledi na kueleweka.
Comments