Mtu na Utu
- Anord Jovin
- Sep 17
- 3 min read
Na mwandishi wetu
Mtu na utu ni maneneno yenye maana tofauti, mtu ni binadamu na utu ni hali ya kuyaishi matendo yanayomfaa mwanadamu, matendo yanayoendana na thamani au hadhi ya mtu.
Thamani ni heshima na katika maisha, binadamu anayo haki ya kuheshimu na kuheshimiwa na kila mtu, hii ni kutokana na kila mtu kuwa na fikra na imani yake ambayo inaweza kutofautiana na mtu mwingine na kutakiwa kuziheshimu iwapo hazivunji sheria na haki za binadamu.
Kutokana na hali ya maumbile, tabia na kiburi cha mali au cheo watu hujisahau na kujikuta wao wakijiaminisha kuwa siyo sehemu ya watu wanaotakiwa kuwaheshimu wengine na badala yake wao ndio wanaotakiwa kuheshimiwa.
Kutokana na nguvu waliyonayo wamekuwa wakipelekea hali hii kudumu na kuonekana yakawaida katika jamii zetu, mfano hali ya kuonekana mwenye fedha ana uwezo wa kumfanyia chochote asiyenacho na mtendewa bila kufanya chochote kudai haki yake na kuhisi ni haki kufanyiwa hivyo.
Nikasimuliwa na rafiki yangu,
Siku moja akiwa katika utekelezaji wa majuku yake ya kikazi akakutana na mtu mmoja ambaye kwa haraka haraka hakumtambua akamuhoji anafanya kazi gani eneo alilokuwepo ambalo anadai ni la wazi na watu wanapita barabarani, akamueleza kuwa nipo kazini.
Rafiki akauliza kwa nini anahojiwa hivo? Yule jamaa akamjibu unajua unaongea na nani? Rafiki akamjibu vivyo hivyo yakuwa na wewe unajua unaongea na nani?
Anasema baada ya mzozano wa muda mfupi wakaja wafanyakazi wenzake ambao alikuwa akifahamiana nao na walivyomuona wakamsalimia na yule jamaa akabaki anashangaa.
Baadae ndipo wakatambuana yakuwa kila mmoja alikuwa katika utekelezaji wa majukumu yake lakini shida ililetwa na mmoja kati yao kutokumuheshimu mwenzake kwa kuzungumza naye kwa ustaarabu na badala yake kuja na kauli ya “unanijua mimi ni nani?”
Yawezekana kwa kazi yake halimuona rafiki yule si chochote si lolote hivyo hatakiwi kumuhoji wala kuzungumza naye chochote.
……..Unanijua mimi ni nani? Hapa ndiopo kuja kitu ninachotaka tuelimishane msomaji wa Montessori Tanzania
Ni kauli ya kibaguzi, kauli ambayo inatweza utu wa binadamu, kauli inayoonyesha kuwa kwa mamlaka yako, cheo chako, mali zako na umri wako ndio una haki kuliko mwenzako.
Kauli hii inaondo amani baina ya watu wawili na kumfanyia muulizwa kujiona hana thamani kabisa, lakini kiburi cha kinywa kutamka hivyo ni kusahau kuwa anayeulizwa yawezekana ameweka utu mbele kuliko cheo, mali au mamlaka lakini ni mkubwa kuliko muulizwa.
Tunachotakiwa kutambua kuwa tulichonacho ni watu mengine yanaweza kundoka muda wote, lakini pia hata vipisipoondoka lakini tutambue tulivyonavyo pia ni kwa sababu ya watu maana yangu hapa ni kwamba kile kinachokufanya ulinge kwa kuona mwenzako hafai kabisa kukugusa wala kukuhoji vinatokana na watu hao hao.
Mfano mwalimu upo kwa sababu ya mwanafunzi, muuza umekuwa muuza duka kwa sababu ya mteja, umekuwa mwajiri kwa sababu ya mwajiriwa, umekuwa daktari kwa sababu ya mgonjwa, umekuwa jirani kwa sababu ya watu wanaokuzunguka.
Umekuwa dereva kwa sababu ya abiria, mvuvi kwa sababu ya walaji, mwenye nyumba kwa sababu ya wapangaji na kadhalika.
Hii ina maana ya kwamba hakuna anayeweza kuishi pekee yake pasipo kumtegemea mtu mwingine kwa namna moja ama nyingine na kama ni hivyo basi yatupasa kuheshimiana ili kuepusha migogoro inayoweza kuleta athali.
Kabla ya kuchukua maamuzi yako binafsi jaribu kufikiri Zaidi ya mara moja ili kujua ni athari kiasi gani itampata mwenzako kiakili na kimwili lakini pia inaweza kukugharimu kiasi gani huko mbaleni.
Kesho yako inahitaji watu Zaidi kuliko chochote, kwani bila watu yawezekana ukawa na chochote kisikusaidie.
Kila mtu akitekeleza wajibu wake kwa usitaarabu na kwa heshi pasipokuulizana “Unanijua mimi ni nani? Na badala yake mkajuana bila kutumia kauli hizi inaweza kutengeneza mahusiano mema kati yanu na kupata rafiki mpya.
Yawezekana baada ya mzozano wa rafiki na jamaa, kuanzia hatua ya upatanisho aliyeuliza unajua mimi ni nani ndiye aliyepata madhara zaidi ya kisaikolojia kuliko mhojiwa lakini kabla ya upatanisho alijiona wa thamani zaidi ya rafiki.




Comments