top of page

AFCON 2027, fursa ya utalii Zanzibar

Na Anord Kailembo


Sekta ya Utalii nchini Tanzania ni moja ya sekta muhimu inayotoa mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi, Tanzanzia imebarikiwa kuwa na vivutio vingi vya asili kama vile mandhari za kuvutia, maeneo ya kihistoria na ya kiakiolojia, hifadhi zenye wanyamapori wengi na baionuai mbalimbali, fukwe zisizochafuliwa na wingi wa utamaduni wa makabila 158.


Nyanda za juu za kusini na kaskazini zina safu nyingi za milima ya kuvutia hasa yenye urefu wa kati ya mita 500 mpaka mita 1,000 katika maeneo yaliyoizunguka; Mlima Kilimanjaro wenye urefu wa mita 5,895 na Meru mita 4,500 inayopatikana kaskazini mashariki mwa Tanzania ni milima iliyotokana na milipuko ya volkano mia ka mingi iliyopita.


Pia maliasili nyingine ni pamoja na ziwa Viktoria, ziwa la pili kwa ukubwa duniani na chanzo cha mto Nile.


Mwambao wa bahari una urefu wa zaidi ya kilomita 804 pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba ambavyo kwa pamoja vinaunda Zanzibar na kisiwa cha Mafia na visiwa hivyo vina mkusanyiko wa vivutio vya asili, utamaduni, historia na akiolojia.


Leo hii tunaangazia namna zanzibar ilivyojipanga kunufaika kiutalii kuto kana na nchi hiyo kupokea baadhi ya timu za nchi za Afrika zitakazoshiriki mashindani ya AFCON mwaka 2027.


Utalii ni moja ya kitu kinachoitambulisha Zanzibar limwenguni kote na hii ni kutokana na kuwa na vivutio vingi ukiachana na uwepo wa vivutio vipatikanavyo habarini, Zanzibar inavyo vivutio vya asili sambamba na kutunzwa kwa vivutio vya kale.


Mamia ya watalii kutoka nchi mbalimbali Duniani uzuru visiwani Zanzibar kujionea vivutio hivyo ambavyo husaidia Zanzibar kufahamika nchi mbalimbali lakini pia kuinua uchumi kuanzia wa mwananchi mmoja mmoja hadi taifa.


Kwani watalii wanapokwenda Zanzi bar huitaji huduma mbalimbali kwa kipindi wanacho kuwepo na huduma hizo hupatikana kwa wananchi, wadau na serikali na hivyo makundi hayo yote kunufaika na uwepo wa watalii hao.


Katika kuhakikisha sekta ya utalii inaendelea kukua kupitia wizara ya utalii na mambo ya kale Serikali ya Zanzibar ilianzisha kamisheni ya utalii ambayo pamoja na mambo mengine jukumu lake ni kuutangaza na kuuendeleza utalii wa kiutamaduni na kimazingira, kupanga na kuendeleza utalii kwa mu jibu wa sera na mikakati ya kimaendeleo ya Serikali, kuandaa shughuli ambazo zitasaidia katika kutangaza utalii wa ndani, kikanda na kimataifa pamo ja na kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa sekta ya utalii kwa uchumi wa taifa na kujuza juu ya majukumu na wajibu wao katika maendeleo ya utalii nchini.


Akizungumza wakati wa uzinduzi wa uwanja wa aman Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dr. Hussein Mwinyi alisema kuwa uwanja huo unaotambuliwa na shirikisho la mpira wa miguu Afrika CAF utakuwa miongoni mwa viwanja vitakavyotumika wakati wa michuano ya AFCON itakayoandaliwa mwaka 2027 kwa ushirikiano wa nchi za Tanzania, Kenya na Uganda.


Anasema uwepo wa wageni wanaokuja kushiriki mashindano hayo ni fursa ya kipekee kwa Zanzibar kutangaza utalii na kwamba wazanzibar wajipange kuhakikisha wanaonesha ukarimu pamoja na kutangaza vivutio vya utalii na kuchangamkia fursa za kiutalii zitakazojitokeza.


“Ni fursa ya kipekee kwa Zanzibar kuonesha ukarimu wa wazanzibar pamoja na kutangaza vivutio vya utalii vya nchi hiyo pamoja na fursa za biashara na uwekezaji kwa uchumi wa nchi” alisema Rais Mwinyi.


Aloyce Protace ni mchambuzi wa masuala ya kijamii na michezo anakiri kuwa Tanzania kuhusika katika kuandaa michuano ya Afcon itakuza sekta ya utalii akidai kuwa yatajumuhisha mataifa mbalimbali ya Afrika ambapo pamoja na kikosi cha wachezaji wa nchi husika pia wapo mashabiki wa takaoambatana na timu.


Anasema Zanzibar imejaaliwa kuwa na vivutio vingi vya kihistoria na timu zitakazopangwa huko zitapata fursa ya kuvishuhudia na kuvitembelea na kwamba kuvitembelea huko mbali na kuchangia pato pia itasaidia kuwa na taarifa za uwepo wa vivutio hivyo ambazo watazipeleka kwao na hivyo kuwa na mwendelezo wa watalii kuingia Zanzibar.


“Naishauri serikali ya Zanzibar kufanya maandalizi ya kutosha katika sekta hiyo na pengine kuanza mapema kutoa matangazo yanayolenga kuifahamisha Afrika juu ya fursa za kiutalii zilizopo ili mataifa yatakayopata fursa ya kwenda huko yajipange” anasema Aloyce.


Anasema unahitajika ushirikiano wa pamoja kati ya serikali ya Tanzania na Zanzibar kupitia wizara zinazosimamia utalii na michezo kuanza maandalizi mapema maana miaka iliyosalia sio mingi.


Kwa upande wake mchambuzi wa michezo Shafii Dauda anasema michezo yenyewe ni utalii tosha kwani huwalazimu watu kutoka maeneo tofauti kufika kujionea hali ya ushindani iliyopo lakini nje ya uwanja ushuhudia vitu vingine ambavyo vinaweza kuwa vya kiutalii.


Anasema ni sahihi kabisa kuwa Zanzibar itapata nafasi ya kukuza utalii maana wapo ambao watapanga safari ya kuja kushuhudia mishindano hayo lakini msukumo wao mkubwa ikiwa ni kufika Tanzania kujionea vivutio vya kipekee katika nchi hiyo.


“Wakifika Tanzania wapo wa takaotamani kushuhudia viswa vya Unguja na Pemba, historia yake wengine watataka kuuona mlima Kilimanjaro au hifadhi ya Serengeti na kad halika” anasema Dauda


Ni sahihi kabisa kuwa mashindano ya AFCON ni fursa tosha kwa Tanzania kutangaza fursa za utalii zilizoko nchini na kuanzia hapo inaweza kuchochea ongezeko zaidi la watalii nchini wanaotokea nchi za kiafrika.


Lakini pia kwa sababu michuano hiyo inafuatiliwa na wadau wengi wa michezo Duniani kile kitakachoonekana kupitia michezo hiyo ndicho kitakachoitanga za Tanzania hivyo kama taifa linaweza kuiweka ajenda ya utalii kuwa kipaumbelee ili wanaofuatilia michuano hiyo moja vya kwa moja ama kwenye vyombo habari waweze kushawishi kana kufika kwenye vivutio hivyo

 
 
 

Comments


bottom of page